Baada ya hili tungojee taarifa rasimi ya maprofesa wawili tegemeo la chama nao kupata kauli zao rasimi ...BONGOAFRIKA ITAKUJUZA YOTE
Subject: KUJIUZULU MAKAMU MWENYEKITI (BARA)
Salaam,
Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu
Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na
Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi
ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda
ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa
marafiki.
Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka
mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika
vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita
bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo
lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa
mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki wa kupindukia.
Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe
Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo
wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu
uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama
kuwa Mali binafsi
Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu
katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu
Nawasilisha.
Said A Arfi (mb)
Nakala Vyombo vya Habari
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment