Thursday, November 21, 2013
Mh. BLANDINA NYONI HATARINI
Kama nilivyohaidi, nimeendelea kuwasiliana na watumishi wa Wizara ya Afya na wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu Ufisadi wa Blandina Nyoni. Yafuatayo ni baadhi ya vitendo vya Ufisadi vya Mama huyu ambaye kwa wengine wanamuona kama mchapa kazi hodari asiyekuwa na doa na anaezuia mianya ya wizi:-
1. Amekuwa akijilipa mshahara wa ziada kupitia Mradi wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) wakati tayari serikali inamlipa mshahara wa ngazi ya Commissioner kupita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
2. Ametengua utaratibu rasmi wa kila Idara ya Wizara ya Afya kuwa na afisa manunuzi wake badala yake ame centralize kwake mwenyewe. Kwa maana hiyo, manunuzi yote ya Wizara anamlazimisha (Comand) Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi kumpa kazi zote ndugu yake anaeitwa Donatha Koko.
3. Amekuwa akicomand wizara kununua uniform za madereva, suti za sikukuu (Sabasaba na Nanenane) na Maua kutoka Mariedo bila kushindanisha na muuzaji mwingine kinyume na kanuni za manunuzi.
4. Katika mikutano yote inayofanyika Wizarani, amekuwa akicomand kampuni ya Kaliula Catering Services kupewa tenda ya kulisha chakula washiriki tangu alipotua Wizarani kama Katibu Mkuu.
5. Miezi mitatu iliyopita aliiteua kampuni ya Soft tech ambayo yeye ni mbia kwenda kukagua Accounts System ya Muhimbili kinyume na kanuni za kikaguzi kwa kuwa tayari ana ‘Conflict of Interest’
6. Amekuwa akiongoza Wizara kwa kutumia Informers ambao kazi yao kubwa ni kumpelekea habari nani anasema nini na nani anasema nini kuhusu yeye binafsi na uongozi wake. Informers wake wakuu ni Elias Mkumbo ambaye ni dereva na Donatha Koko ambeye ni ndugu yake wa damu damu na ni afisa ugavi wa wizara
7. Amemkopesha gari la serikali aina ya Suzuki Informer wake Elias Mkumbo (dereva) ambae kimsingi hastahili kukopeshwa gari kutokana na cheo chake. Kwa dereva wa serikali, anachoruhusiwa kukopa ni Baiskeli, Piki piki na Piki piki ya miguu mitatu (Bajaj)
8. Amenunua vingamuzi vya magari (Vehicle Security and Fuel control system) vibovu kwa ajili ya magari manne kwa shilingi 1.3 Billion bila kufuata taratibu za manunuzi kwa kucomand Single source procurement kutoka kampuni moja yenye makao yake huko Israel. Manunuzi haya yamefanyika wakati Hospitali nchini zikiwa hazina dawa, Interns doctors hawajalipwa mishahara yao, watumishi wake wakidai fedha za likizo, uhamisho na vyuo vingi vya afya vilivyo chini yake vikiwa na madeni lukuki.
9. Mwishoni mwa mwaka wa fedha 2009/2010 alihamisha kiasi cha Shilingi 1,968,475,931 mali ya Wizara ya Afya kwenda National Institute for Medical Research (NIMR) bila kibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizi zilikuja kuhojiwa na CAG katika ripoti yake ya serikali kuu ya mwaka 2009/2010
10. Mwishoni mwa mwaka huo huo wa fedha alihamisha kiasi cha Shilingi 3,083,400,000 mali ya Wizara ya Afya kwenda Health Sector Development Project bila kibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizo pia zilihojiwa na CAG.
11. Amelikosesha Taifa kupata fedha za Mfuko wa dunia mzunguko wa 11 (Global Fund Round 11) kwa kupitia Mradi wa Taifa wa kudhibiti Malaria Nchini (NMCP) kwa kushindwa kutumia fedha zote zilizotolewa na mfuko huo katika mizinguko ya nyuma. Kwa kifupi ni kwamba Global Fund hawatoi pesa wakiona una Significant unspent balances.
12. Amekuwa akizuia uhamisho wa Chief Accountant (Bi Helen Saria Mwakipunda), Chief Internal Auditor (Bi Anna Joseph Mhere) na Director of Adminstration and Personnel (Bi Tabu Chando) kwa kile anachodai wanamsaidia katika utendaji wa Wizara. Amezua barua za uhamisho za Chief Accountant mara mbili, Chief Internal Auditor mara moja na Director of Administration and Personnnel mara moja. Ukweli ni kwamba amekuwa akizua uhamisho wa wakurugenzi hawa kwa sababu ni watu waoga na wamekuwa wakikubali chochote anachosema hata kama kinavunja kanunu na taratibu za serikali mfano katika maeneo ya Manunuzi.
Kwa nini Chief Accountant (Hellen Saria Mwakipunda) na Chief Internal Auditor (Anna Joseph Mhere) wanamuogopa kama Mungu Blandina Nyoni? Ni hivi: Hellen Mwakipunda, alikua Junior staff kwa Nyoni, kipindi hicho Nyoni ni Mhasibu mkuu wa Serikali. Blandina Nyoni ndiye aliye mpandisha cheo Mwakipunda na kuwa Chief Accountant, kipindi hicho hata CPA hakuwa nayo. Anna Mhere alipata u-CIA akiwa na Advance Diploma in Accountancy - ADA tu. Ili swala lilikuwa linawashangaza watu wengi sana. Sasa kwa inferiority complex walizokuwa nazo hawa wakina mama, ni lazima wamuabudu Blandina Nyoni.
13. Amemuhamisha aliyekuwa Kaimu wa Kitecho cha Ugavi Mzee Funga kwenda Hospitali ya Mirembe Dodoma kwa kukataa kununua Uniforms, suti na Maua kutoka kwa Mariedo kwa sababu alihoji ni kwa nini Mariedo watoe huduma wakiwa hawana Mkataba na hawajashindanishwa na wauzaji wengine.
14. Amekuwa akihama hama na dereva wake toka Hazina alipokuwa Muhasibu Mkuu wa serikali hadi Wizara ya Maliasili na Utalii kama Katibu Mkuu. Pia amehama na dereva huyo huyo kutoka Maliasili hadi Wizara ya Afya kinyume na taratibu na kanuni za Utumishi wa umma ambazo haziruhusu kiongozi au mtendaji yeyote wa serikali kuhama na dereva au / na secretary
15. Hamsalimii Naibu wake Waziri Bi Lucy Nkya kutokana na Naibu huyo kugoma kupangiwa dereva ambaye ni Informer wake. Hadi leo hii hamsalimii hata wakikutana kwenye kordo. Kinachowazungumzisha ni madokezo tu.
16. Alikuwa na uhusiano mbaya na Naibu Waziri wake aliyeondoka Bi Aisha Kigoda kwa sababu ambazo hazijulikani. Kama ilivyo kwa Lucy Nkya nae pia walikuwa hawasalimiani.
17. Akiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, aligombana na Waziri wake Bi Shamsa Mwangunga na wakawa hawasalimiani hata wakikutana kwenye kordo
18. Alipokuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali alikuwa anateua ndugu zake na watu anaofahamiana nao na kuwapa vyeo vya u Chief Accountants na Chief Internal auditors bila kuwa na sifa kamili ya kupewa vyeo hivyo. Mfano kuhold CPA (T) na Masters.
19. Amesababisha kushuka kwa morali ya utumishi kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Hivi sasa ndiyo Wizara inayoongoza kwa kuwa na watumishi wengi walioamua kwenda likizo ya masomo ili kuepuka manyanyaso yake.
20. Ameanzisha utaratibu ndani ya Wizara ya Afya wa kupokea Excheque kutoka hazina na anazihold bila kufanya distribution kwenye idara zake. Kutokana na utaratibu wake huu anafanya malipo kwa kutegemea mahitaji yanavyojitokeza. Utaratibu huu ni kinyume na kanuni za hazina za matumizi ya fedha za umma.
21. Ikitokea kazi za Construction na maintanance anacomand tenda ipewe kwa Mzenzi Contractors Ltd. Alishinikisha Mzenzi ajenge ofisi za Wizara zilizopo Dodoma na akafanikiwa, baadae alishinikiza Mzenzi ajenge jengo banda la Maonyesho la Wizara kwa ajili ya Nane nane lilipo Dodoma na akafanikiwa na alishinikiza Mzenzi apewe tenda ya kufanya small maintanance wizarani kwenye ofisi yake, Ofisi ya Waziri na Naibu Waziri kwa ajili ya kuweka tiles na kuboresha vyoo na akafanikiwa.
22. Katika section ya Matibabu ya nje amejenga Network na Hospitali za India ambazo zinapelekewa wagonjwa kuibill wizara inflated invoice prices.
23. Amechukua mashine za kusafishia figo akishirikiana na Dk Linda Ezekiel pamoja na reagent na filter wakazipeleka Msasani kwenye Hospitali yao ambayo Blandina Nyoni ana shares.
24. Amejenga banda la maonyesho ya sikukuu ya nane nane kwa kutumia fedha za NIMR kwa Shilingi 1.5 billion. Lakini banda lenyewe lililopo pale Nane nane Dodoma ukiliangalia tu kwa haraka haraka kwa macho thamani yake haizidi hata million 400.
25. Ameingiza robo tatu ya vifaa bandia vya vipimo vya Ukimwi kutoka Korea Kusini.
26. Ameingiza kinyemela bila kufuata taratibu za Manunuzi kampuni ya kufanya usafi ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.
27. Ameshinikiza kampuni ya Jambo Concept Tanzania Limited kupewa tenda namba ME/007/2009-10/HQ/G/191 kwa ajili ya Printing and Placing of Billboards with TB/TBHIV bila kufuata taratibu za manunuzi. Kwa maelezo zaidi juu hii tenda soma maelezo kutoka 'someone' kama nilivyoyaatach hapa chini baada hii orodha
28. Blandina Nyoni akishirikiana na Dr Deo Mtasiwa wamecheza mchezo mchafu katika tenda ya ununuzi wa Bajaj kama ilivyoratibiwa na Wizara ya Miundombinu kupitia tenda namba ME/015/2009 - 2010/S/06. Katika tenda hiyo bajaj moja ilinunuliwa kwa US$ 8,400. Kwa maelezo zaidi juu hii tenda soma maelezo kutoka kwa 'someone' kama nilivyoyaatach hapa chini baada ya orodha hii.
29. Ametengua uteuzi wa Dr Mtimba kama Mkurugenzi Msaidizi na kumuhamishia Damu Salama Tabora na badala yake amemkaimisha Dr Budeba kwa miaka miwili mfululizo bila kumthibitisha kushika nafasi hiyo kinyume na taratibu za utumishi. Anafanya hivyo kwa sababu Dr Mtima hana urafiki naye.
30. Ametengua uteuzi wa Dr Sawe ambaye angeenda India kuwapokea Wagonjwa na badala yake kamteua Dr Goroka ambaye kiudugu ni mtu na Mama yake. Hivi sasa kampeleka Dr Ngoka ambaye ni family friend wake pia.
31. Ametengua uteuzi wa Dr Sawa anayesimamia uandikishaji / usajili wa Hospitali binafsi na kumpatia Mtoto wa Balozi Lusinde ambaye ni rafiki yake na walisoma nae High School Kilakala mmoja akiwa Form V mwingine akiwa Form VI
32. Ametengua uteuzi wa Dr Muhame ambaye alikuwa Msajili wa tiba asilia na kumpatia Dr Naomi ambaye ni Mama Mdogo wake. Yaani yeye na Blandina ni mtu na mtoto wa binamu.
33. Yeye ndiye chanzo cha masahibu yaliyowakabili Watanzania kwa kukosa huduma ya afya kwa zaidi ya Wiki mbili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kitendo chake cha kutaka kulipiza kisasi kwa Intern Doctors kwa kuwahamishia Mikoani pale walipodai haki zao ambazo ni stahili zao halali.
Note: Orodha itaendelea kuongezwa kadri tunavyozidi kupata data kwa watu walio karibu na Wizara za Afya, Maliasili, Hazina na Muhimbili
From 'someone'
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment