skip to main
|
skip to sidebar
RAIS KIKWETE ATISHA NCHINI Sri Lanka
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete azungumza kwa ajili ya viongozi wenzake Sri Lanka
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amesema kuwa maoni ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kuhusu
ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 yatakuwa mchango mkubwa kuhusu
nini kifanyike baada ya kumalizika kwa kipindi cha Malengo ya Maendeleo
ya Milenia (MDG).
Aidha, Rais Kikwete ameipongeza nchi ya Sri
Lanka kwa kuandaa vizuri na kwa mpangilio mzuri Mkutano wa Wakuu wa Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) uliomalizika mchana wa leo,
Jumapili, Novemba 17, 2013.
Rais Kikwete ameyasema hayo na
kutoa pongezi hizo usiku wa jana, Jumamosi, Novemba 16, 2013, wakati
alipotoa Salamu za Shukurani kwa niaba ya viongozi wote waliohudhuria
Mkutano huo kwenye Chakula cha Usiku rasmi kilichoandaliwa na Rais wa
Sri Lanka, Mheshimiwa Mahinda Rajapaksa kwenye Ikulu ya Temple Trees ya
nchi hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake, Rais
Kikwete amesema: “Mada ya mwaka huu ya mkutano wetu wa CHOGM ya
Maendeleo ya Pamoja kupitia Ukuaji wa Pamoja imekuja kwa wakati unaofaa.
Kwa taasisi kama ya kwetu ambayo inawakilisha watu bilioni mbili
kujadili suala hilo hasa kwa kutilia maanani mjadala unaoendelea kuhusu
ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 ni jambo la busara sana.”
Mkutano wa CHOGM ambao ulianza juzi, Ijumaa, Novemba 15, 2013,
umemalizika leo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kumbukumbu ya Bandaranaike
mjini Colombo, Sri Lanka.
Akizungumzia mkutano huo, Rais
Kikwete amesema: “Tunakupongeza Mheshimiwa Rais kwa maandalizi mazuri ya
Mkutano huo. Tunajua siyo kazi rahisi kuandaa Mkutano wa ukubwa huu.
Lakini kwa uongozi wako wa busara na uongozi wako, kwa kusaidiana na
Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, kila kitu kimekwenda vizuri.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Kwa niaba ya viongozi wenzangu waliokusanyika
hapa jioni ya leo, napenda kukutakia wewe, Mheshimiwa Rais, kila la heri
katika uendeshaji wa taasisi yetu hii.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Novemba, 2013
No comments :
Post a Comment