Friday, November 22, 2013

MWIGURU ANENA KUHUSU ZITTO .Soma hapa

  Mh. MWIGULU NCHEMBA MBUNGE WA IRAMBA AMETOA YAKE YA MOYONI JUU YA SAKATA LA ZITTO MSOME HAPA


Kuvuliwa vyeo kwa Zitto Zuberi Kabwe na Dr Kitila Mkumbo kutakuwa na visingio vingi, ukweli ni kwamba "NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATAWALA AKILI KUBWA" It is natural kwamba akili ndogo ikitawala akili kubwa,
1) Yatatumika mabavu na nguvu nyingi kuizuia akili kubwa kupanda juu,
2) Zitatafutwa sababu nyingi na visingizio uchwara kuhalalisha kuizima akili kubwa tofauti na vigezo vya hoja kwakuwa akili ndogo haiwezi kuizidi akili kubwa kwa hoja,
3) Hutumika vitisho vingi kuzuia akili kubwa kuchukua hadhi yake
4) Akili ndogo ni rafiki wa akili ndogo mwenzake, hivyo akili ndogo huzungukwa na akili ndogo kwakuwa ushauri wa akili kubwa akili ndogo hushindwa kutumia ama kushindwa kuonesha umiliki mbele za watu. Kwenye chadema wenye akili wote wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo. Pale bungeni watu wanaoweza kufundisha na waliokuwa wakifundisha hata unaibu waziri kivuli hawapati kwakuwa wanatumia akili zaidi badala ya nguvu. Lakini walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya chadema kwakuwa wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na matakwa mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa. Vijana wahitimu wa vyuo wanaopenda siasa waliandikiwa barua kuwazuia kuhutubia mkutano wowote wa hadhara sawasawa na matakwa ya akili ndogo inapotawala akili kubwa. Zito, Kitila, Christowaja, Matiko, Opulukwa, Baregu, Leticia, Selasini, Arfi, Akunay, Naste wengi wao MA holders kwa chadema ni rejects. Ukiwa mwanafamilia au ukoo au kazi au wito maalum wa viongozi ndio utakwepo kwenye list. I know Zitto tangu tukiwa chuoni, he is a brilliant and consistent politician, namjua Dr Kitila tangu chuoni, he is resourceful. Hivi kosa walilofanya ni kubwa kuliko mchango wao waliofanya kwenye kuwajenga watanzania kuwaamini vijana kwenye siasa? Je kosa lao ni kubwa kuliko mchango wao unavyohitajika? Vijana tuko kazini na wakati huohuo tuko mafunzoni. Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi. Haya ndio madhara ya AKILI NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA, HOFU NDIO HUTAWALA

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2013. BongoAfrica - All Rights Reserved.