Thursday, November 21, 2013
MWIGAMBA AMETEKWA / AMEWEKWA KIZUIZINI?
Kwa mara ya mwisho kuongea na huyu kaka yangu na rafiki yangu Samson Mwigamba ilikuwa siku alipokuwa hospital akipata matibabu baada ya kundi la akina Lema kumpiga kwenye kikao cha chama cha kanda ya Arusha,
Siku tatu baadae kila nikijaribu kupiga simu zake zote naambiwa huduma kwa mteja huyu imesitishwa kwa muda.... nimejitahidi kuwauliza rafiki wengine nao wanajaribu hali ni kama hiyo hiyo.
Je mwigamba kama ameamua kusitisha namba zake zote ni kwa nini? au je hajui sisi marafiki zake tunakuwa na wasiwasi kwa kupotea kwake hewani tena kwa kujibiwa kuwa huduma zake zimesitishwa kwa muda?
Kwa mujibu wa utaratibu wa mawasiliano ikiwa mtu atazima simu bado unaweza kufanya tracing na ukajua GPS za mahali alipo na hiyo simu. lakini ukisitisha huduma kama hivyo, huwezi juwa mahali alipo mtu huyo.
Sasa napata mashaka kwa sababu watekaji mara nyingi huwa wanaweza kufanya hivyo kwa namna wajuavyo hasa wakiwa na connection na watu wa mitandao ya simu makao makuu,
Hii nimeamua kuitoa hapa ili tusaidiane kuwaza, je ametekwa au amewekwa kizuizini je kama ni hivyo nani kafanya hivyo?
NAMBA ZAKE NI HIZI........... PIGA UJIBIWE NAWE..........0713953761/ 0767953761
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
sasa huu umbaya
ReplyDelete