"NITAGOMBEA URAIS TANZANIA 2015 NIKIWA MGOMBEA BINAFSI, SITAKI KUFUNGWA NA VYAMA VYA SIASA" MUNISHI
Mwimbaji wa nyimbo za injili anaetisha afrika ya mashariki na kati kwa uwezo mkubwa wa uimbaji na ubunifu katika kufikisha ujumbe uliokusudiwa, Mchungaji Faustin Munishi, amenukuliwa na BONGOAFRIKA akisema atagombea urais wa Tanzania 2015 kwa tiketi huru bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa,
Mtumishi huyu aliyetisha sana mwaka 1998 na album yake iitwayo MALEBO yuko nchini kenya baada ya vitishi vingi anavyodai kuvipata toka kwa serikali baada ya kuimba wimbo uliitwa ccm imezeeka na kuhamia kenya.
Amesema hana raha kuona mambo yakiwa hovyo katika nchi yake na yuko tayaru kuomba ridhaa ya wanachi ili awatumikie bila ufujaji wa mali za umma kwani amejaa hofu ya Mungu.
hapa chini namnukuu
''Nitagombea Urais bila siasa Sababu mimi siyo mwanasiasa
wala sipendi Siasa.
Naomba Watanzania wanipe nafasi ya kutoa mchango wangu ili wote
tusaidiane kuweka mawazo pamoja jinsi gani tuiongoze nchi yetu kufikia
maemdeleo ya kumaliza hali duni za maisha na kuinua kiwango cha maisha''
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment