BONGOAFRIKA inamshukuru sana Mh. DAVID KAFULILA kwa kujitokeza na kupangua maneno yaliyotengenzwana watunzi wa HEKAYA FEKI, kwanza niseme nilipoona hii post JF nilishangaaa
sana na kuitafakari hata kama ni kweli una feeling hizo kwa ninavyokujua
usingeweza kutamka hadharani hvi, lakini nikaiona hii inarudiwa tena
na tena na kwa bahati mbaya
sikufanikiwa kukusikia ukikanusha, juzi nilipoiona tena JF nikaamua
kuileta hapa ili angalau tusikie labda utatokea hadharani kuisemea kwa
kuikazia au kuikanusha ....ASANTE KWA KUMALIZA UTATA HUU..NAOMBA NIIFUTE
SASA
MSOME HAPO CHINI ........
Kufuatai kutapakaa mitandaoni kwa kauli zilizoanzia katika mtandao wa JF na baadae kusambaa kwenye mitandao mingine ya kijamii,
Zilizowekwa kana kwamba zinamnukuu Mbunge wa kigoma kusini David Kafulila akisema kuwa Rais 2015 lazima atokee kigoma, zikiwananga wabunge waliosimamamajukwaani kule kigoma na kutoa kauli za msisitioz juu ya kumuunga mkono rais atakaegombea Urais 2015 akitokea kigoma.
Wabunge hao walizikana kauli zao baada ya kurejea tokea safari ile waliyoifurahia na kuserebuka majukwaani pamoja na wabunge wa kigoma katika tamasha lililoandaliwa na wabunge hao.
Habari hiyo ilitoa maelezo ambayo ukiyasoma vyema utagundua kuwa yamepikwa kama kawaida ya wapikaji wasio na umakini, kauli nyingi katkati ya tamko feki zimekaa kihekaya zaidi ya kifact
Mbunge huyo wa Kigoma kusini David Kafulila (NCCR- Mageuzi) ameibuka na kusema kuwa watu wanaofanya hivyo wana lao jambo na kama kawaida yao wakiiishiwa hoja za kuruka nazo katika vijiwe vyao vya siasa za kutembelea nyota za watu watazusha lolote tu juu ya mtu ili wapate cha kunywea kahawa.
Akiongea na BONGO AFRIKA AMESEMA......
''Wandugu
haya ni matumizi MABAYA ya social media.
Sijawahi kusema Mimi kwamba
rais ajaye lazma atoke Kigoma .
Siasa za urais na makundi ya urais
upinzani na ccm nazichukia sana.
Sasa kuna watu wanataka kulazimisha tu
niseme wanavotaka wao au ambavyo wangependa
kusikia kwa lengo la kushusha heshima yangu, sikupenda, haya maneno
yaliwekwa Mara ya kwanza kwenye mtandao wa jamiiforums.
Nilihuzunika
sana, sijui aloweka kwani wengi wanatumia majina bandia.
Niliwasiliana
na mmiliki wa mtandao huo baadae kutaka kujua kwanini wanaruhusu posts
ambazo hazina source?
Badae alikiri na tangu hapo kwenye aliweka ujumbe
jf kuwa mtu yeyote mwenye tatizo awasiliane nae na akaweka email yake
pale.
Niwambie wazi watanzania Kafulila mnaemsikia sio mwanasiasa
mpuuuzi wa kusema maneno ya kijinga kiwango hicho.
JF huwa nasoma tu,
naweza kuchangia labda kwa mwaka Mara mbili kwasababu sipendi namna
baadhi ya wachangiaji wanavotumia kejeli, matusi, wapo wachangiaji
wakiandika napenda kusoma lakin sipendi kuchangia.''
Aliendelea kusema.......
''Nimeamka asbh nakuta
link inayosema Mimi David Kafulila Nilisema rais ajaye lazma atoke
Kigoma.
Story hii ilipata kuandikwa na mtu mmoja kwenye mtandao wa
jamiiforums , bahati mbaya aliandika bila source.
Yani alizuka tu na
kuandika maneno ambayo Angetamani yaonekane Mimi nimesema, bahati mbaya
alitumia jina bandia.
Niliwasiliana na mmiliki wa mtandao
huo, na akanielewa kuwa ile story ilikua na lengo lake.
Sijawahi na
singowahi kusema ujinga wa kiwango hicho. Nachukia sana mijadala ya
urais inavokwenda nchi hii.
Nashukuru mmiliki wa jamiiforums alinielewa
na kutoa.
Mimi jamiiforums huwa nikichangia labda Mara mbili kwa mwaka,
lakin sipendi kuchangia kabisa.
Huwa napita kusoma tu kwani kuna baadhi
ya watu napenda kusoma maandiko Yao.mtu aloweka maneno yale alikuwa na
malengo yake kwasababu zake hasa ili kunivunjia heshima niomekane
nafikiri kidogo.
Tusijadili rais atoke wapi wala awe nani, tujadili
issues ambazo zinahitaji kushughulikiwa ndipo tuone nani ataweza sio kwa
misingi ya eneo, dini,Kabila wala rangi Bali uzalendo na uwezo wake''.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment