Wananchi hao wa jijini Kampala walikusanyika baada ya kumuona Kiongozi wa Chama cha upinzani cha FDC Dr Besigye akitembea kwa miguu na hivyo kuanza kumfuata.
Tukio hilo limesababisha vurugu kubwa hasa baada ya wananchi kuimba nyimbo za kumsifu Dr Besigye kama shujaa wao na kusisitiza kumuondoa Mseven madarakani.
Dr Besigye alikamatwa na kuzuiliwa katka kituo cha polisi kwa zaidi ya saa 3 jijini kampala.
Hali hiyo ilisababisha wananchi kufanya vurugu na kulazimisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya kwa mabomu ya moshi.
Ikumbukwe kuwa Mseven alimpiga marufuku Dr Besigye kutembea mitaani kwa kila alichokiita ni kuchochea wananchi kufanya vurugu.
Source : BBC SAWAHILI
No comments :
Post a Comment