Tuesday, November 19, 2013

WAZIRI SITTA AMVAA LOWASSA NA KAPUYA



Mmoja wa wafuatiliaji wa siasa za Tanzania aishie ughaibuni amenukuliwa katika akaunt yake ya twitter akimpongeza Waziri sitta kwa kauli zake za hapo jana
 ''Kitu ambacho kinanifanya nampenda sana Sitta ni mwanasiasa anaweza kuzungumza anachokiamini bila woga. Gazeti la Tz Daima la leo uk wa 4 linaripoti hivi:

Mh Sitta jana alikuwa anazungumza katika mahafali ya kidato cha nne shule ya Agape Seminari , Marangu Moshi anasema:''

" Nchi imefika pabaya kama viongozi wanaweza kutoa vitisho na tambo za watoto wao kuuza dawa za kulevya huku vyombo vya dola vikishindwa kuchukua hatua". " Nchi imegawanyika makundi ambapo baadhi ya viongozi wamekuwa na kiburi cha kutamba kwamba hawawajibiki kwa vyombo vya kisheria". Sitta alitoa mfano wa Waziri mstasfu ambaye sasa ni mbunge, aliyeripotiwa na vyombo vya habari kumtisha mtoto aliyemtuhumu kwa kumbaka mara mbili alipoitwa kwake kuchukua ada. Alisema polisi hawajachukua hatua hata ya uchunguzi tu na kubaini kwamba Tanzania ni nchi kubwa haiwezi kuendeshwa hovyo hivyo tu, na kwamba lazima iendeshwe kwa viwango vya maadili vitakavyoleta maendeleo.

Kuhusu Lowassa anasema:

" Watu walianza kujipambanua miaka miwili iliyopita kwa harambee mbalimbali kwa baadhi ya makanisa, misikiti na sehemu nyingine" Hesabu ya fedha hizi kwa kipindi cha miaka miwili ni kiasi cha sh bilioni 7" Anasema mtu huyu na kundi lake wakipewa nchi wataiangamiza na kwamba watapora nchi kwa kasi na hatimaye misingi ya umoja na usawa itabomoka na kulitumbukiza taifa kwenye machafuko.

Big up Mh Sitta kwa kusema ukwel

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2013. BongoAfrica - All Rights Reserved.