Wajumbe wa Bunge maalum waomba rushwa.
Sms hii nimetumiwa saa 11 alfajiri,........ ''IKO HIVI BILA 500,000/= HATUUNGI MKONO HOJA YA SERIKALI MBILI, BALI TUTAUNGA MKONO HOJA YA SERIKALI TATU''
Kwa mujibu wa CUF ndio walitoa msimamo wa serikali tatu wakiwa na uhakika wa kunufaika na ushindi watakaoupata huko zenji kwani ikiwa serikali tatu zitakubalika CUF itashinda lazima, na ndipo cdm ikapima na kuona hoja yao ya awali ya serikali moja haiwezi kuzaa matunda nao wakuunga mkono serikali tatu, ccm nao wametangaza msimamo wao kuwa wanaunga mkono serikali mbili zenye maboresho sio tatu.....
Sasa hawa wajumbe wenye kudai posho, inamaana kwa ujumbe wao huu wanamaanisha wanasukumwa na nguvu ya pesa, upande utakaokata pesa nzuri kwao ndio wataounga mkono, ni aibu sana.
Je ikiwa Cuf watatoa pesa nzuri kwao wataunga mkono hoja ya serikali tatu, na pesa ikiongezwa wataunga mkono hoja ya serikali mbili....huu ni upumbavu kwenda bungeni bila kuwa na uwezo wa kupembua mambo na kuwa na misimamo ya mitazamo yako eti utegemee nguvu ya pesa ikusukume.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment