UCHAFU WA MATOKEO WABUNGE WANAHUSIKA
Pamoja na kupewa mwongozo
wa alama za viwango vya ufaulu, lakini baraza la mitihani limetangaza
matokeo yakiwa yamejaa kasoro nyingi na zinazotia aibu kubwa.
Ukianza kusoma matokeo hayo baadhi ya shule utashangaa sana, kama kweli
walioyapanga walikuwa wanafanya hivyo kwa kukusudia tu au walipitiwa kwa
bahati mbaya.
Katika alama za
ufaulu kimadaraja, mwanafunzi mwenye alama wa wastani wa alama 40
amewekewa division zero lakini wengine katika shule hiyo hiyo wenye
alama 40/41...45 wamewekewa division three, huku wengine wa alama 40
wakiwa na three bado kuna wenye alama 36/39 wamewekewa zero.
ukiringanisha alama zao za walio na 40 inayosomeka kama zerowamepata
c,d,d,c,e,e,f...wakati wenye alama 43 zinazosoeka three/four wana
e,e,e,e,f,f,f...nimewashangaa sana,
Lakini mwisho nikakumbuka
migomo ya mwaka jana ya madaktari na walimu walipopaza sauti kupinga
ongezeko la posho za wabunge wetu, wabunge wetu wakajifanya kuipotezea
hoja hiyo huku wakiendelea kulamba posho hizo na wengine kujaribu
kupinga na kutoa kisingizio kuwa zinzwekwa kwenye acc zao moja kwa moja
hivyo hawawezi kurudisha kwa kuwa pesa ni pesa ni tamu ukiipata
unasahau,
Sasa wahaeshimiwa wa baraza wamefanya makusudi ili
waitwe tena kuyapanga upya ili walipwe posho kwa awamu nyingine,hii yote
ni matokeo ya wabunge wetu kuwa walafi na wanafiki..
Linapofika swala la posho bungeni hakuna mtu anaeonekana kupinga kwa
shingo ngumu kama wanavyofanya wanapotaka spika apinduliwe..ndio unafiki
mkubwa unaosababisha na kuzaa majanga.
Tazama aibu ya nchi
hii...kesho utawaona wabunge wanafiki wakianza kukosoa matokeo haya
wakisahau wao ndio chanzo cha haya yote.
Mtazamo wangu huu wala msijenge chuki..jipimeni.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment