Sunday, November 17, 2013

UHURU & RUTO, WAKO KONA YA KIPIMO CHAO....ICC!

UN WALIPOKATAA KUONDOA KESI YAO ICC IMEIFANYA KENYA KUWAJUA ADUI ZAO
 

 Je iamii ya Kimataifa ni Adui wa Kenya? Kwa nini wawe adui wakati wao ndio waliomtuma Koffi Annan kuwaleta Pamoja wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi? Je yule aliyesaidia Kenya mkaunda Serikali ya Mseto ya Kibaki na Raila iliyotaka kesi zifanyike Kenya lakini Bunge la Kenya wakapinga muswada huo wakisema kesi zipelekwe ICC leo amekuwa adui kukubaliana na kauli ya Bunge la Kenya wakati huo? Iliyokuwa kesi ya watu binafsi sasa imekuwa ni kesi ya Kenya inashitakiwa ICC? Mbaya zaidi Afrika inaburuzwa iingie kwenye kesi hiyo ili sasa iwe kwamba kuwashitaki Ruto na Uhuru ICC ni kuishitaki Africa? Ni kweli hiyo au viongozi Africa wameonyesha jinsi walivyo wabinafsi? JAMII YA KIMATAIFA IKITUACHA WENYEWE AFRICA HATUTACHINJANA KAMA KUKU KILA SIKU? MUSEVENI NA KAGAME WANAOSEMA TUACHWE WENYEWE MBONA WAMESHINDWA KUTATUA MZOZO WA CONGO?

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2013. BongoAfrica - All Rights Reserved.