skip to main
|
skip to sidebar
SIASA ZA LEO NA FALSAFA YA ''UHITAJI WA RIKA''
''SIASA ZA LEO NA FALSAFA YA UHITAJI WA RIKA''
Napotazama mihemko ya kisiasa kwa vijana kushabikia siasa/wanasiasa kipindi hiki!
Nakumbuka falsafa ya ''UHITAJI WA RIKA'' niliyoibuni mwaka 2012 na
kuiweka kwenye kurasa za KITABU CHANGU kiitwacho ''UTASHI NI
MTU''......falsafa inasema..
''Kuna wakati rika fulani huibuka na
mihemko inayofanana kwa muda wa wakati wao kushabikia au kuiga na
kufanya kitu/jambo fulani linalofanana, lakini rika la wakati wao
likipita kila kitu hupita kisha huja rika jipya na mihemko yao mipya juu
ya kitu kipya.
Karibia 60% ya rika lao hushabikia kitu cha aina
moja, rika hili nalo hupita na huja rika jipya lenye mihemko ya uhitaji
wake pia.
Ukomo wa rika huja tu pale tabia zenye kufanana miongoni
mwa rika hilo huanza kuhama na kila mmoja kufuata njia yake kimawazo na
kifikra, hakuna ukomo wa umri katika tabia za uhitaji wa rika''.
By Grayson M Nyakarungu UTASHI NI MTU (2013)..........''
Nijadili falsafa yangu kwa mifano hai,
Tukumbuke miaka ya 1998 -2006 enzi la Kuibuka kwa makundi ya Muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania kundi kama vile:-
KWANZA UNIT, SAREHE JABIR(Solo Artist na mwanzilishi wa rap ya
kiswahili), TWO PROUD (kwa sasa Sugu aliyeufanya muziki huu kupiga hatua
ya kuanza kuuzwa), WATEULE,WABABE CRAK, GORILA KILLERS, HBC(Nigga
Jay,Terry Fanani na Bigie Willy) , kundi la DIPLOMAT (saigoni na
wenzake) n.k,
Nimetaja makundi na wasanii wa muda mrefu kidogo
waliokuwa na dhamira kubwa ya wazi ya kuona Muziki wa kizazi kipya
Tanzania unakuwa imara na wenye tija, baadae kizazi kile cha muziki
uliokuwa wa dhamira ya kutengenza mfumo wa muziki kilipita kikaibuka
kizazi cha rika la wasanii wa upepo wanaoenda na matukio walioamini si
muda wa kuimba matatizo ya jamii bali ni muda wa kuburudika tu na watu
wasahau shida zao kwa muda, miaka hii tunakumbuka kulikuwa na mihemko ya
vijana wakiibuka na kufanya muziki wa kizazi kipya (kwa sasa bongo
fleva).
Kila mkoa, kila wilaya, kila kata, kijiji na pengine
karibia kila kaya usingekosa mtu anaejiita msanii, anaesuka nywele bila
kujali jinsia yake, anaevaa jeans kwa mtindo wa KK, anaetembea amekunja
bega moja na hata waliovuta bangi sio kwa sababu ya asili yao bali kwa
sababu ya mihemko ya kudhania kuwa kuwa msanii lazima uvute bangi.
Bongo fleva iliwatoa wengi kimaisha, kiumaarufu, hata kimaslahi mengine waliyoyajua wenyewe, mradi tu iliwatoa.
Wakati ule kila msanii aliyetoa single redioni tulitarajia na baadae
tukashuhudia tamasha kubwa la uzinduzi wa album yake, kwa wengi kipindi
kile walipoingiza sokoni album waliuza sana, kipindi hicho walisambaziwa
na kampuni moja tu ya wahindi (GMC) iliyoko kariakoo inamilikiwa na
MMAMU,
Waliuza sana tapes (kanda) na walitoka kwa kweli, na
wengi wao mie nilishiriki harakati zao kimuziki ikiwa ni pamoja na
kutengeza beats zao katika studio kadhaa hapo bongo miaka ya 2003 -2005
na wengine kutumia mashairi yangu niliyowapa kwa hiyo nawafahamu na
ninaujua muziki wa bongo vilivyo.
Lakini kizazi cha rika
kipoondoka hatukuona tena kitu kinaitwa uzinduzi wa album pale Diamond
jublee wala club billcans, wala tour za mikoani za kutangza album hazipo
tena, mbaya zaidi hata tapes hazikuzalishwa tena ukiachilia
kutonunuliwa kwake,
Hii ni dhahiri kuwa wafanyabiashara walisoma
alama za nyakati kuwa rika lao la biashara halipo tena, hata Mr Nice
aliwahi kukiri kuwa nyimbo za TAKEU hazina soko tena kwa sababu
waliokuwa wakizipenda ni watoto wa enzi zile na sasa wameshakuwa watu
wazima na haoni umuhimu wa kuimba tena nyimbo hizo kwani hazina soko.
Kilichobaki kwenye huu mziki ni wasanii tu lakini sio wale mashabiki
wala wateja wa awali, hivi sasa wasanii kwa kujua kuwa hakuna wateja nao
hawana mpango wa kuuza kazi zao bali wanauza show tu, ''nipe pesa
nipande jukwaani niimbe, acha watu wakopi nyimbo zangu kwenye flash disc
zao wasikilize popote ili wawe oriented na nyimbo zangu nipate show''.
Katika siasa za sasa za dunia yote wala sio Tanzania tu, mihemko hii ya uhitaji wa rika imetia fora.
Napenda kuwaomba vijana watambue kuwa kwenye hii mihemko ya uhitaji wa
rika ni mizuri endapo tutaitumia vizuri, tukadumu nayo kwa ari
tuliyonayo kwa mwelekeo wenye dira na ndoto sahihi kwa Taifa letu.
Wakati ule wa Bongo sanaa, niliwahi kushudia mashindano ya mfalme wa
rymes, wakati Afande Sele the King (moja ya wasanii wanaotumia akili
sana kuandika mashairi na kuufanya muziki wao kutokushaka thamani) wa
MOROGORO aliibuka kidedea.
Wakati ule kila kijana alikua akishabikia
msanii anaempenda, ilifikia hatua wasanii wakawa na ugomvi baina yao na
kuwafanya mashabiki wawe na ugomvi wa kiushabiki kama wale
wanaowashabikia.
Kadhalika kwenye siasa hivi sasa hakuna tofauti na wakati ule vijana wanadhani siasa ni burudani kama ilivyokuwa sanaa.
Siasa ni mfumo wa kutengenza mbele ya Taifa, tutofautiane kifikra,
kimtazamo na kiitikadi lakini tusitofautiane kwenye lengo kuu
(kutengenza Taifa imara).
''Uwe na malengo yako, yenye utofauti na ya mwingine, lakini yote yalenge kutimiza lengo kuu - ''UTASHI NI MTU'' Ukurasa wa 44.
Wapo wasiojua tofauti ya vyama vya siasa na Taifa au Serikali, hawa
wapo tayari hata kupinga Jakaya Kikwete kuitwa Rais, wapo pia wanaodhani
tofauti ya itikadi ndio tofauti ya malengo makuu ya siasa za nchi
(wanahitaji shule)
Wapo wanaodhani kuibadili nchi kimfumo wa utawala
ni kuondoa chama tawala na kuweka kingine bila transformation ya fikra
na mfumo wa utawala ndani ya jamii na ndani ya vichwa vya watu
wanaojiita/wanaojidhania ni viongozi, (hapa shule kubwa sana
inahitajika, lakini tukienda kwa lengo la kuitoa ccm tu madarakani kwa
aproach ya now and then,tukidhania kuwa lengo letu namba moja ni kuitoa
ccm madarakani bila kujali jamii haina wala haijajua tofauti ya taifa na
vyama vya siasa, bila jamii kubadilishwa kimtazamo na kiwajibu, bila
mifumo ya kiuongozi kubadilishwa, kesho ataibuka mwingine na kuwahadaa
kwa style hiyo hiyo na tutajikuta tunajipeleka shimoni)
Mwisho wa yote tunajikuta tumekusanya watazama show na wacheza show kwenye makundi ya siasa.
Watazama show wakikosa ladha ya burudani waliyotarajia huondoka bila
kujali wamelipia kiingilio getini, huamua kurudi kulala wakitajia kuota
ndoto zenye kuwatia moyo, kuliko faraja waliyoitegemea na kuikosa kwenye
show,

Wacheza show wao ni wabaya sana, maana wao hucheza
sambamba na msanii anapoimba jukwaani, msanii hujikuta akiendeshwa na
wacheza show walio kwenye dancing flow ambao hata hakufanya mazoezi ya
show pamoja nao, wacheza show huamua hata kumlazimisha msanii aimbe
wimbo fulani ambao hata hakujiandaa nao, (Mtakumbuka 2006 Shaggy
alipokuja diamondo jublee kilichotokea)
Hawa maDisco Bugerz wakikosa kuheshimiwa na msanii kwa kile wakitakacho huamua kupiga fujo na hata kumrushia chupa au matusi...
Mifumo ya kiutawala ni lengo namba moja, kubadilisha mifumo
inayosababisha wizi wa mali za umma, mianya inayosababisha rushwa,
mianya inayosababisha uonevu n.k
Sio kuahidi kuwafunga watu au
kuwachukulia hatua wenye tuhuma za wizi huku mifumo ikibaki vilevile, je
uhakika wa kupata watu waaminifu kwenye mifumo iliyowapa watangulizi
wako mianya ya wizi uko wapi?
Huwezi kuamini katika mabadiliko
ya mtu pasipo mfumo kubadilika kwanza, tunatamani kuona viongozi
wanaodhani wanaweza kuwa mbadala wa hawa waiopo wakijipambanua kwa
mifano halisi ya nafasi zao walizo nazo katika taasisi zao kwanza.
Mjue kwa sasa watazama show ni wengi kuliko wacheza show, hawa watzama
show huwa makini sana na endapo utaenda nje ya key watajua na hawatapiga
kelele, ukirudia tena watajiuliza..je ni makusudi au kajisahau, au
katuona tumekuja humu kumshangaa yeye na sio show?
Wakianza kujiuliza maswali hayo uwezekano wa kuondoka bila kujali muda wao waliopoteza kwako ni mkubwa mno.
Wacheza show wao watakuzomea na pengine usipojirekebisha watakupiga na kukuabisha.
Siasa haiko hivyo bali tunasimama leo kwa ajili ya kesho, na sio
kusimama mchana wa leo kwa ajili ya jioni ya leo, Mobb politics huvuma
kwa wakati wa rika na huisha rika linapokwisha.....!!
NATAMANI RIKA LA UHITAJI HILI LITAKAPOPITA TUBAKI KWA LENGO MOJA KUU NALO NI KUJADILI NA KUPANGA KWA AJILI TAIFA LETU
No comments :
Post a Comment