Wednesday, November 20, 2013

MWIGAMBA HAFUKUZWI CHADEMA..!.Soma hapa hisia za huyu bwana!!

 

BONGOAFRIKA, imekutana na habari hii ya mtu anejiitaN Chris Lukosi kwenye mitandao ya kijamii akimkaribisha Kamanda Mwigamba huko CCM, nachukua nafasi hii kuwahakikishia hakuna mwigamba ataefukuzwa chadema kwa kosa la kuandika mitandaoni maoni yake,
Hata kama ni kosa basi kosa hilo halitamuacha salama Lema Mbunge wa Arusha aliyetumia njia kamahiyo kumtukana Naibu katibu mkuu wa chama na kwenda kinyume na msimamo wa kambi ya upinzania ya kupinga posho badala yake yeye akaonekana kuitetea na kuililia.

Viongozi wa Chadema hawataweza kufanya upuuzi huo wakamfukuza mwigamba wakimuacha lema.
Na hata kama akiondoka chadema hawezi hamia ccm nasema kwa niaba ya kaka yangu huyu ninaemuheshimu sana.

SOMA HAPA ALICHOANDIKA ... Chris Lukosi

''Ndugu zanguni,

Napenda kuchukua nafasi hii kumkaribisha shujaa Mwigamba nyumbani kwani tayari sote tunajua kondoo hawezi jichanganya na fisi

Sote tunajua mwigamba alipigwa kwa sababu alihoji kwa nini fisi wanakula nyama yote buchani hadi kigogo cha kukatia nyama na ndipo alipopata kipigo nusura na yeye achanganywe na hiyo nyama

Karibu Shujaa Mwigamba

Rudi Nyumbani CCM ambako sote tunajua ile hadithi ya mwanampotevu, yalipomkuta aliruidi nyumbani na dhambi zake zikasamehewa

JITAMBUE!''

1 comment :

 
Copyright © 2013. BongoAfrica - All Rights Reserved.