(Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori nchini,Jonh Muya)
Wakati
wanyama wakiwamo tembo wakiendelea kupotea kwa kuuawa kwa wingi na
majangili katika hifadhi na mbuga mbqalimbali za taifa nchini, imeelezwa
kuwa, wahalifu hao wamewekeza kwenye biashara hiyo haramu.
Akizungumza
na paparazi wetu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Kaimu Mtendaji Mkuu
wa Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori nchini, Jonh Muya, alisema majangili
wamewekeza kwenye biashara hiyo haramu kama ilivyo kwa wale
wanaojihusisha na dawa za kulevya, kwani imevuka mipaka ya nchi na
mtandao wake ni mkubwa ndiyo maana imekuwa ikileta shida hata katika
kukabiliana nayo.
Kwa mujibu wa
Muya, matajiri ndiyo wahusika wakuu wa vitendo hivyo vya ujangili huku
wakiwatumia walalahoi kwa ajili ya kuwachukulia mizigo yao kutoka kwenye
hifadhi au mbuga za wanyama na kuipeleka maeneo walikoamriwa.
Akizungumzia
tukio la kukamatwa kwa meno ya tembo takribani 1,000 Zanzibar mwanzoni
mwa wiki iliyopita, Muya alisema tatizo hilo pia linaweza kuchangiwa na
uwapo wa bandari bubu nyingi katika ukanda wa Bahari ya Hindi huku
zikiwa hazina udhibiti maalumu.
Alisema
kuanzia Bandari ya Tanga hadi ya Dar es Salaam kuna takribani bandari
bubu 46, ambazo kwa namna moja au nyingine, hufanya udhibiti wa vitendo
vya ujangili kuwa mgumu na kutokana na hiyo inawawia vigumu hata kujua
bandari ipi ambayo meno hayo yalipitishwa hadi kwenda kukamatwa
Zanzibar.
Alisema
vita dhidi ya ujangili inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ukosefu
wa teknolojia ya kisasa katika kudhihiti uhalifu huo.
Hata
hivyo, alisema wana mipango mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na
vitendo hivyo ambavyo vinalenga kuliporomosha taifa kiuchumi kwa kukosa
watalii, ikiwamo kuwa na vifaa vya kisasa kama boti na kushirikiana na
nchi nyingine ili kupeana uzoefu wa namna wanavyokabiliana na ujangali
kwenye sekta hiyo.
No comments :
Post a Comment