Wapo wanaodhani kuibadili nchi kimfumo wa utawala ni
kuondoa chama tawala na kuweka kingine bila transformation ya fikra na mfumo wa
utawala ndani ya jamii na ndani ya vichwa vya watu wanaojiita/wanaojidhania ni
viongozi, (hapa shule kubwa sana inahitajika), lakini tukienda kwa lengo la
kuitoa ccm tu madarakani kwa aproach ya now and then, tukidhania kuwa lengo
letu namba moja ni kuitoa ccm madarakani bila kujali jamii haina wala haijajua
tofauti ya taifa na vyama vya siasa, bila jamii kubadilishwa kimtazamo na
kiwajibu, bila mifumo ya kiuongozi kubadilishwa, kesho ataibuka mwingine na
kuwahadaa kwa style hiyo hiyo na tutajikuta tunajipeleka shimoni.
Haitakuwa tofauti na wasanii waliopata hasira kwa
kuona unyonyaji umezidi katika sanaa na kuwahamasisha wasanii wenzao kuanzisha
movement kubwa ya kupigana na wanyonyaji, lakini katikati ya vita vyao
wakatokea wajanja zaidi yao waliotumia njia kama yao na kuwahamisha wasanii
wenye ushawishi kasha movement yao ikafia mbali.
Mwisho wa yote tunajikuta tumekusanya watazama show
na wacheza show kwenye makundi ya siasa.
Watazama show
ni watu wenye ufahamu kuhusu sanaa au muziki, ao hukaa au husimama kando
bila kucheza wala kelele zozote, hutamani kumwona msanii akiimba na kucheza kwa
kiwango halisi, asiende nje ya ufunguo wa kuimbia, sauti isikwame wala asianze
kukohoa hovyohovy jukwaani.
Hutamani kumwona msanii akianza kutumbuiza mwanzo
mpaka mwisho bila kuonesha dalili ya kuchoka ili mradi tu atimizia hitaji la
kuimba kwa kiwango kinachostahili, ndiyo raha ya watazama show nikiwemo mimi.
Endapo msanii akikosauwezo huo niliouleza hapo juu,
pengine kwa kukohoa, watzama show hudhani amepaliwa tu na anaweza kukaa sawa na
kuimba vyema, au akienda nje ya mstari wa ufunguo huwa wavuimilivu na
hujitengenezea sababu zao za kujifariji na kutegemea atarudi kwenye ufunguo na
ataimba vyema.
Lakini akidumu katika uhafifu huo wa kimuziki,
watazama show huanza kuguna na pengine hujiuliza kama msanii anafanya makusudi
au hayuko serious na kazi yake.
Mara wanashangaa msanii anaishiwa pumzi na kuanza
kulazimisha wanyanyue mikono hewani akiwaambia…mikono… mikono…mikono… hali hii huwakera watazama show na huamua
kuondoka bila kujali muda wao na gharama walizotumia kufika hapo, wanaamua bora
wakalale kuliko kukwazika.
Watazama show wakikosa ladha ya burudani
waliyotarajia huondoka bila kujali wamelipia kiingilio getini, huamua kurudi
kulala wakitarajia kuota ndoto zenye kuwatia moyo, kuliko faraja waliyoitegemea
na kuikosa kwenye show,
Kadhalika kwenye makundi ya wanasiasa wapo wasanii
hodari wa kuyamudu majukwaa kuanzia kwenye hoja mpka kwenye propaganda, kwa
kundi la watazama show kwenye muziki kwenye siasa tunawaita wachambuzi wa hoja
za kisiasa, hawa hujali sana kuona mtu anaeongelea issues na sio propaganda
pekee na kusahau kutoa suluhu ya matatizo hata kama yeye sio serikali lakini
jukwaa ni sehemu ya yeye kutolea ushauri kwa serikali akichanganya na propanda
ili angalau wananchi wamwone anafaa.
Huyu mwanasiasa akienda nje ya ufunguo huu huwapoteza
watazama show wa kisiasa na hubaki na wacheza show kama nitakavyoelezea hapa
chini.
Wacheza show wao ni wabaya sana, maana wao hucheza
sambamba na msanii anapoimba jukwaani, msanii hujikuta akiendeshwa na wacheza
show walio kwenye dancing flow ambao hata
hakufanya mazoezi ya show pamoja nao.
Wacheza show
huamua hata kumlazimisha msanii aimbe wimbo fulani ambao hata hakujiandaa nao,
(Mtakumbuka 2006 Shaggy alipokuja diamond jubilee kilichotokea)
Hawa maDisco Bugerz wakikosa kuheshimiwa na msanii
kwa kile wakitakacho huamua kupiga fujo na hata kumrushia chupa au matusi.
Kadhalika kwenye siasa kuna kundi hili la wacheza
show wanaopenda kusikia mwanasiasa akiwananga wanasiasa wenzake kwa zaidi ya
dakika sitini (60) au zaidi akitembelea nyota au maneno ya wenzake au makosa ya
wenzake kila jukwaa haongelei issue zaidi ya Fulani alisemakitu hiki au kile,
au mimi nitapambana na Fulani mpaka ang’oke au Fulani ni mwizi au fisadi au
serikali imekosea hiki bila yeye kusema nini kifanyike.
Wacheza show wa siasa hufurahi sana kila anapoongea
kwa namna hii, lakini ipo siku wanakutana nae huyu mwanasiasa aliyezoea
kutembelea nyota ya wenzake akakosa kuwanga hapo wacheza show ya siasa huanza
kusema siku hizi huyu jamaa akachuja hana kasi kama zamani, kumbe kilichobadilika
ni kwamba leo ameongelea issues na sio watu hapo ladha yao waliyoizoea hupotea
kabisa.
Hali hii imesababisha wacheza show wengi kuwa wafuasi wa wanasiasa wa aina ya
kizazi cha akina feruz wasiowaza kuhusu mabadiliko ya mifumo, ni wanasiasa
wanaowaza katika kubandua mwanasiasa Y na kuweka mwasiasa X bila kuchora upya
msitari wa utawala na mfumo wake.
Inatokea wakati wansiasa wa aina hii wanapata wakati
mgumu majukwaani au kwenye mijadala wanapokutana na wenye hoja kinzani
zinazojadili issues badala ya wao kujaribi kujibu hoja kwa hoja hubadilika na
kufanana na wasanii wa kizazi cha akina Diamond wanapoishiwa pumzi utawasikia
wakisema ..weka mikono juu…oyoooo… mikon
mikono mikonooo…
Na kwa sababu wacheza show wanapenda aina ya hamasa
aliyonayo msanii huinua mikono juu na kumpigia makofi kwa shangwe kubwa.
Lakini hufikia wakati mashabiki hawa kwa kuwa
hawajajengwa kimfumo huhama na kumfuata msanii mwingine atakaekuwa na hamasa
kubwa zaidi ya huyu kwani wao wanachokifuata ni hamasa na sio msingi wala
mfumo.
Kwa tafasiri rahisi wanasiasa hawa huhama kwenye
mada na kuanza kwenda na aina ya usemaji waliozoea majukwaani kwa kuwataja watu
na kuanza kutafuta kupigiwa makofi na wananchi ya kishabiki.
Hata kwenye siasa pia hufikia mahala wacheza show wa
siasa wakamwona mwanasiasa mwingine mwenye domokaya kali zaidi na mwenye
Kiswahili cha pwani namisemo ya umakuini na bi kilembwe na kumfuata wakimwacha
wa awali kwa sababu wanataka nahau na vijembe vipya sio mfumo wala misingi.
Mifumo ya kiutawala ni lengo namba moja, kubadilisha
mifumo inayosababisha wizi wa mali za umma, mianya inayosababisha rushwa,
mianya inayosababisha uonevu n.k
Sio kuahidi kuwafunga watu au kuwachukulia hatua
wenye tuhuma za wizi huku mifumo ikibaki vilevile, je uhakika wa kupata watu
waaminifu kwenye mifumo iliyowapa watangulizi wako mianya ya wizi uko wapi?
Huwezi kuamini katika mabadiliko ya mtu pasipo mfumo
kubadilika kwanza, tunatamani kuona viongozi wanaodhani wanaweza kuwa mbadala
wa hawa waiopo wakijipambanua kwa mifano halisi ya nafasi zao walizo nazo
katika taasisi zao kwanza.
Mjue kwa sasa watazama show ni wengi kuliko wacheza
show, hawa watzama show huwa makini sana na endapo utaenda nje ya key watajua
na hawatapiga kelele, ukirudia tena watajiuliza..je ni makusudi au kajisahau,
au katuona tumekuja humu kumshangaa yeye na sio show?
Wakianza kujiuliza maswali hayo uwezekano wa
kuondoka bila kujali muda wao waliopoteza kwako ni mkubwa mno.
Wacheza show wao watakuzomea na pengine usipojirekebisha
watakupiga na kukuabisha.
Siasa haiko hivyo bali tunasimama leo kwa ajili ya
kesho, na sio kusimama mchana wa leo kwa ajili ya jioni ya leo, Mobb politics
huvuma kwa wakati wa rika na huisha rika linapokwisha.....!!
NATAMANI RIKA LA UHITAJI HILI LITAKAPOPITA TUBAKI
KWA LENGO MOJA KUU NALO NI KUJADILI NA KUPANGA KWA AJILI TAIFA LETU
No comments :
Post a Comment