KAMATI TENDAJI YA CLUB YA SIMBA 'WANAMSIMABZI' IMEMSIMAMISHA MWENYEKITI WA KAMATI YA CLUB HIYO BWANA ADEN RAGE.
Kamati tendaji imekutana leo katika ofisi yake eneo la kariakoo na kufanya maamuzi hayo baada ya kujiridhisha na taarifa za kiutafiti zinazoelezea uhafifu wa uadilifu wa Bwana Aden Rage.
Tukio hilo limekamilika muda wa saa 11:30 Asubuhi ya leo katika ofisi hiyo.
Wanachama wa club ya simba wameingia katika hali ya sintofahamu baada ya mgawanyiko mkubwa wa makundi mawili makubwa kila kundi likiwa na hitaji lake.
Mzozo umetokea kati ya mashabiki wanaounga mkono hatua hiyo na wengine wakipinga
Bwana Aden Rage hajapatikana kuelezea namna alivyopokea uamuzi huo.
Source: Radio One Breaking news.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment