Mwaliko wa Mkutano na Waandishi wa habari: Ndugu Albert Msando
MWANASHERIA wa Mhe Zitto Zuberi Kabwe (Mb), Dr. Kitila Mkumbo na Samson
Mwigamba, Ndugu Albert Msando, atazungumza na wahariri wa vyombo vya
habari katika Hoteli ya Serena kuanzia saa nne na nusu asubuhi (saa 4.30
asubuhi).
Dhima ya mkutano huu
itakuwa kutoa ufafafunuzi juu ya mashitaka 11 na majibu yake ambayo
Mhe. Zitto Kabwe na washitakiwa wenzake walipewa na Kamati Kuu ya
CHADEMA. Aidha, katika kikao hiki Ndugu Msando, kwa niaba ya wateja
wake, ataeleza hatua ambazo wateja wake wanazichukua ndani ya chama
katika kuhakikisha kwamba mgogoro uliopo unakwisha kwa amani na haraka
iwezekanavyo bila kuleta athari zaidi kwa chama.
Tunatanguliza shukrani na tunaomba waalikwa wazingatie muda.
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe,
Jumanne, 10 Desemba 2013
Dar es Salaam
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment