RIPOTI KAMILI...MH ZITTO KABWE (MB) APEWA ULINZI MKALI WA SIRI NA JESHI LA POLISI!
*Awasilisha mashtaka polisi
*
Asema wanaomtishi watakamatwa
JESHI la Polisi limempa ulinzi wa siri Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe (CHADEMA) kama njia ya kumkinga asidhuriwe na maadui wake katika siasa.
Hatua hiyo ya polisi imechukuliwa siku chache baada ya mwanasiasa huyo kijana na mama yake mzazi, Shida Salum, kwa nyakati tofauti, kudai kuwa Zitto amekuwa akiwindwa na watu ambao wamekuwa wakitishia uhai wa wake kutokana na siasa zinazoendelea ndani ya Chadema.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, kiliiambia RAI kuwa uamuzi huo ulifikiwa katika kikao wiki iliyopita, baada ya jeshi hilo kupata taarifa za tishio la kudhuriwa kwa kiongozi huyo kwa kile kilichoelezwa kuwa tofauti baina yake na viongozi wenzake wa Chadema.
Kikao hicho ambacho kiliwahusisha makamishna kutoka makao makuu ya jeshi hilo, kilipitia kwa kina taarifa ya kutaka kudhuriwa kwa Zitto kwa kutofautiana msimamo na viongozi wenzake ndani ya chama hicho.
“Kikao kilifanyika Novemba 11 mwaka huu ambako pamoja na mambo mengine kimeweza kujadili kwa kina kutaka kudhuriwa Zitto … hivyo walitumwa makachero wa jeshi la polisi waweze kubaini anapoishi.
“Wamefanya kazi hii na sasa kiongozi huyo analindwa kuanzia nyumbani kwake Tabata. Askari maalumu wamepewa kazi ya kuimarisha ulinzi nyumbani kwake hadi katika nyendo zake,” kilisema chanzo hicho ndani ya jeshi la polisi.
Zitto, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, kwa muda mrefu amekuwa akitofautiana na viongozi wenzake hasa katika masuala ya taifa hali inayofanya atafsiriwe kuwa anatumika kutaka kuivuruga Chadema...
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment