Saturday, November 16, 2013
NYAKARUNGU:UONGOZI BILA ELIMU NI UJINGA WA KUTUPWA
Leo ni siku ya jumamosi Niko mapumzikoni:
NASEMA NA WABUNGE MAKANJANJA WANAOENDA NA UHITAJI WA RIKA!
Tujadili suala la elimu ya Rais wa Nchi, zamani hata mie niliingia mkumbo huo wa kusema kuwa uongozi si elimu bali maono na hekima na uwezo tu,
Nami nikatoa mifano ya watu wenye elimu zilizotukuka wasio na uadilifu katika uongozi na wenye tamaa, wenye kutumia elimu zao kuiba kwa kalamu.
Lakini leo nimeujua umuhimu wa shule kwenye uongozi, kwa hili hakuna atakaenishawishi nimchague mgombea wa nafasi asiye na elimu kulingana na ngazi yake anayogombea.
Nimeona namna madiwani wanavyoweza kudanganywa kwenye vikao vya mipango ya halmashauri na kuingia mkenge kisha issue ikigundulika wao huanza kuropoka majukwaani kuwa mkurugenzi mwizi kumbe alipowaeleza kuhusu mipango walikuwa hawaelewi wala uwezo wa kuchambua hawana, hawa nao wanazama kwenye ile falsafa ya mihemko ya uhitaji wa rika.
Nimefahamu namna wabunge wasio na elimu wanavyoteseka kwenye vikao vya kamti zao, aisee ni aibu sana, halafu ukiwakuta majukwaani au wakati wakitoa hotuba mbadala wanavyokimbia msala wakati nao walikuwa kwenye vikao hivyo ambavyo ndio matokeo ya bajeti hiyo.
Kizazi cha uhitaji wa rika ni NGOME YA WAJINGA.
Kuna wabunge wenye juhudi za kutafuta maarifa wao hukusanya watu wenye uelewa wa mambo kabla ya kikao cha kamati, hupewa ushauri na kisha huwa angalau na mchango mzuri kwenye kamati huko ndiko kwenye kupika mipango na sio kwenye bunge pale wengi wanatuzuga tu wanapiga kelele za mbweha asiyeza kukamata sungura.
Wapo wanaodaka posho kisha kukodi hotel zaidi ya 3 na kuwaweka wasichana zaidi kila hotel kisha kupanga zamu za kulala huko na kisha huudhuria kamati kupokea posho tu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment