Friday, November 22, 2013

SAKATA LA CHADEMA KUJITEKA NA KUMWAGIA KUBENEA TINDIKALI 'tutafakari tulinganishe na yaliyotkea na yanayoendelea ...'



Picha:Saed Kubenea.jpg

WANA -BONGOAFRIKA, Leo nimeamua kuwakumbusha watu juu ya mambo mengi yanayowekwa kwenye mitandao nikitaka tuyatafakari pengine ni ya kweli kutokana na uhusiano wa matukio na kile kinachokuwa kimeandikwa kabla.

Mtu aliweka jf habari hii ndefu sana na ile ya sakata la mbowe kupanga mbinu za kumuondoa zitto uongozini na leo yametimia, sasa swali waliopinga na kusema ilitungwa leo wako wapi, je hli la kujiteka na kumwagia saed kubenea tindikali tutabisha kwa kiwango gani? 

Habari kamili ilkuwa hii hapa chini
SAKATA LA CHADEMA ‘‘KUJITEKA’’
NA
SAED KUBENEA KUMWAGIWA TINDIKALI.

Ndugu Wananchi,
Taifa letu la Tanzania linapitia katika wakati wa upevukaji wa uhuru wa kusema kwa uwazi, pia Taifa letu linapitia katika harakati za demokrasia na maozezi ya deomkrasia.

Katika kipindi hiki tumeshuhudia mambo mengi yakitokea ikiwa ni pamoja na baadhi ya watu na taasisi zao kuutumia uhuru huu wa kusema vibaya kwa lengo la kutimiza malengo yao binafsi au kutimiza wajibu wa uhuru wao wa kusema.

Pia tumeshuhudia baadhi ya watanzania wakiitumia vibaya demokrasia na wengine wakiitumia vizuri kwa manufaa ya umma na wengine kwa manufaa yao wenyewe.
Baada ya utangulizi huo sasa nianze makala hii kwa kina na kwa kusema kila kitu ninachokifahamu kuhusu mada hii.

Ndugu Wananchi,
Mimi nimekuwa mtumishi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) toka 2003 nikiwa mwanachama wa kujitolea na baadae 2004/8 nikiwa kiongozi wa chama makao makuu,

Mwaka 2006 secretariat ya makao makuu ilipanga mikakati ya namna ya kukifanya chama kiwe maarufu na namna ya kuwafanya wananchi wakichukie chama tawala ili watafute mbadala wake ambao tulilenga uwe ni chadema.

Katika mikakati ile tuliazimia mambo mawili makubwa yatakayoleta matokeo yote mawili kwa wakati mmoja yaani kukifanya chama kiwe maarufu na wakati huo huo wanachi wakichukie chama tawala ili wajiunge na CHADEMA.

Mkakati namba moja ulikuwa kuandaa timu ya red brigade ya watu wenye weledi wa kijeshi wenye uwezo wa kucheza karete au kong fou ili tuwaandae wawateke viongozi wa taifa wa chama (CHADEMA),

Mkakati ule uliwalenga wabunge maarufu Dr Slaa na Zitto Kabwe, lakini pia ulilenga kumteka Mwenyeikiti wa Taifa Mbowe Alkaeli Freeman. (Lakini haya ya kutekwa viongozi yalipangwa nyuma ya uficho bila dr slaa kuhusishwa kwa sababu maalum nitaeleza baadae)

Ili kulifanya tukio lile lihusishwe na Chama tawala tulipanga yatolewe matamko makali dhidi ya serikali na chama tawala kwa lugha kali itakayosababisha serikali ijibu na ikibidi ijikanganye kutoa kauli ili red brigade watakapotuteka iwe sababu ya moja kwa moja kuwahusisha.

Katika mkakati ule mbinu na namna ya kuwateka viongozi hawa uliandaliwa vyema vijana wakiwa chini ya uangalizi wa mlinzi wa Mbowe aliyetolewa tarime (kwa jina la Chacha suguta) wakipewa mafunzo namna ya kutokomea baada ya kuwateka viongozi wetu na kuwapora computa na simu zao  bila kuwadhuru.

SIKU YA TUKIO
Tukiwa makao makuu mida ya saa 3 asubuhi tukingojea muda wa matamko kutolewa na viongozi wa chama, alikuja Marehemu Chacha Wangwe akiongozana na kijana aliyekuwa mahili sana kwa siasa za tarime Chacha Okong’o aliyeshinda kura za maoni kugombea Ubunge jimbo la Nyamagana lakini akaondolewa na wenje akapewa nafasi yake kwa misingi ya Mbowe kuogopa damu ya marehemu chacha wangwe ingeweza kumrudia mapema sana endapo Okong’o angepata nafasi ya uongozi.

Marehemu Wangwe alipoingia na kuambia juu ya tamko lililoandaliwa kutolewa kuisema serikali kuwa imepanga mbinu ya kuwaua Mbowe, Zitto na Dr Slaa, Marehemu alipinga issue hiyo na kuonya kuwa itaweza kukidhuru chama chenyewe kama haikupimwa kabla ya kuitoa,
Wangwe akaonya kuwa sio kila umaarufu huwa na tija,
Mbowe aliwakaripia sana Mnyika na Zitto kwa kumshirikisha Wangwe ambaye yeye alimwita ni mvuta bangi tena akisisitiza kuwa kama ni bangi wengi tunavuta lakini zake ni za wehu.
Kwa misimamo ya wangwe aliyekuwa mbunge wakati huo hajawa Makamu Mwenyekiti wa chama taifa, Mbowe alizuia tamko lile,  waandishi waliokuwa wamealikwa walipofika waliambiwa kuwa kikao kilihairishwa.





MIPANGO YA KUTEKWA YAKAMILIKA.
Mbowe aliwaita vijana wake wa red brigade akiwa na vijana wake wa mipango Mnyika na Zitto(zitto wakati huo akiwa miongoni mwa wanaompinga wangwe kwa nguvu zote bila kujua afanyalo akiwa mkono wa kazi wa Mbowe akiamini kuwa anapambana na wahujumu wa chama kumbe anapambana na demokrasia) ikumbukwe kuwa Zitto aliamua kujitoa kwa mbowe baada ya mbowe kushagilia kifo cha wangwe wakiwa musoma wakitoka msibani, wakiwa hotelini Mbowe alianza kumsema marehemu vibaya akiamini kuwa aliokaa nao wote ni vijana wake, hapo zitto aliinuka na kusema kwa uchungu sana kuwa sikujua kama mwenyekiti unaroho mbaya kiasi hiki, alipomaliza hayo aliondoka na ndio ukawa mwanzo wa mwisho wa uhusiano mzuri wa mbowe na Zitto.

Sasa tuendelee namipango ya kujiteka,
Mbowe akiwa na Zitto na Mnyika  ndani ya ofisi yao makao makuu mitaa ya ufipa, walipanga mikakati ya kuwaita vijana wao walioandaliwa kufanya utekeji bila kumtaarifu katibu mkuu wao wakihofia ataogopa na pengine atatoroka, lakini waliamua kumficha pia ili atakapotekwa na kuporwa computa yake ya mkononi na simu zake kisha mwenyekiti atamwamuru katibu atoe tamko huku akiamini ni ccm wametuma watekaji ilia toe tamko lenye lugha kali kwani walijua akipaniki huwa na hasira na kumwaga maneno mengi ya hovyo kama tunavyomuona akifanya leo.

Ndugu Wananchi,
 Ikiwa ni saa 7 mchana mpango ukiwa umepangwa siku ya jumapili siku waliyoipanga na kuiona ni siku muafaka ya kutekwa, mwenyekiti alimwambia Dr slaa kuwa siku hiyo usiku watakuwa na kikao pale ofsini kwao makao makuu Ufipa kuanzia saa 4 usiku akamuomba ajiandae tu lakini ajenda atakuja nazo yeye, dr slaa alikubali bila kujua kuna nini nyuma ya pazia,

Baadaye Mbowe alimwagiza Mnyika kuwataarifu watekaji kuwa wajiweke tayari,
Mnyika alitekeleza agizo hilo lakini kama kawaida yake alitoa uzuru wa kutokuwepo kwenye tukio kwa kusingizia jukumu la kifamilia,

Ikumbukwe hii imekua tabia yake kwa mlolongo ufuatao;-
Wakati kambi ya upinzani bungeni iliazimia kuondoka bungeni kupinga kumtambua Rais Kikwete, Mnyika yeye aliomba ruksa kuwa anaumwa na hakuingia bungeni kwa uoga wake na kwa kumuonea aibu kikwete kwani kikwete alimchangia Mnyika Tsh 5,500,000/= wakati wa kampeni kwa sababu ya kutompenda hawa ng’umbi ambaye aliingia kwa nguvu za lowassa na ndio maana jk alimteua Nape kuwa mkuu wa wilaya masasi wakati wa kampeni,

Kikao cha kumshughulikia Zitto kilichokaliwa kwa Mbowe kilipoiva Mnyika aliomba ruksa na kuondoka,
Kadhalika na kwenye mpango ule wa kutekwa Mnyika alifanya hivyo (alidanganya kuwa mjomba wake ametoka Botswana na hakuna mtu wa kumpokea bali yeye anategemewakumpokea)

Zitto na Mbowe waliwasili makao makuu wakamkuta Dr Slaa amekaeti akiwangojea,
Mkakati ulikuwa watekwe wote ikibidi wapigwe japo sio kwa kiwango kikubwa cha kuumizwa, wakati wakizugazuga kuisubiri saa6 usiku ifike Zitto alipigiwa simu na mkuu wa kikosi cha watekaji na kuomba pesa za mafuta kwa kuwa gari lao moja limebuma, wakati huo hakukuwa na M-Pesa wala kitu kama hicho,

Mbowe alitoa tsh 200,000/= zitto akapewa apelike msasani walipokuwa, zitto alifikisha pesa kasha akaacha maagizo kuwa wasubiri atakapofika makao makuu atawapa alerting sign.

Zitto alifika makao makuu akamkuta mbowe anajadiliana na Dr slaa kama viongozi wakipanga ajenda za vikao,
Zitto akampa alama ya dole kuonyesha amekamilisha kazi huko huku Dr slaa haju lolote,
Baada ya dakika kadhaa mbowe aliaga kuwa anaenda kutoa pesa kwenye ATM mitaa ya mwanamboka manyanya,

Lakini muda anaaga zilikuwa zimebaki dakika chache sana kabla ya kutimu saa6 muda muafaka kwa kutekwa walikojiandalia,
Mbowe aliondoka na derva wake akiwaacha wajumbe wamekaa ndani ya makao makuu ili hali mpango huu ukiwa unajulikana kwa zitto, mbowe na mimi tu, wajumbe wengine hawakujua kitu, sisi tulijiandaa kisaikolojia lakini nilishangaa kuwaona akina Mnyika na Mbowe wanaanza kutoroka, nikajiuliza je walitoa maagizo kuwa tuuwawe au walitoa maagizo kuwa tuumizwe?

Nikamvuta Zitto kando nikamng’ata sikio juu ya jambo hili nay eye akashituka, wakati huo wale maghaidi feki walikuwa wakipiga simu kutaka kupata ruksa ya wao kuvamia,
Zitto akampigia Mbowe lakini Mbowe hakupokea simu, bali akatuma sms kuwa waambie hao makamanda waje mie nitafika kabla hawajafika,

Nilimkataza Zitto asiwape ruksa hao maghaidi feki kwani yawezekana kuna mchezo umetegwa bila sisi kujua na tunaweza kudhurika kasha tukajuta nae akanisikiliza tukaazimia tumngojee Mbowe arudi kwanza,

Tulingojea kwa muda wa saa nzima mpaka saa 6:40 bila mbowe kufika toka umbali wa kilomita moja ambayo kwa miguu ungeweza kutumia dakika 20 tu,
Mimi niliamua kuondoka kasha zitto nae akanitxt kuwa ameondoka,
Ilipofika saa 8 usiku mbowe alipiga simu kwangu na kuniuliza  kama tuko salama au la!!
Nikamjibu wewe uko wapi mwenyekiti wangu?
Akajibu nilipata mgonjwa ghafla nikampeleka hosp.

Ikumbukwe kuwa mbowe ana tabia ya kuanzisha zogo kasha kuwaachia iwatafune.
Mtakumbuka Mbowe alipowadanganya vijana na Dr slaa wakeshe wakiota moto kuitaka serikali imwachie Lema huko Arusha, lakini Mbowe alitoroka baada ya kuona zogo linawaka moto mkali akamwacha Dr Slaa akakamatwa peke yake na wapambe wao.

Tuendelee na sakata la kutekwa
Usiku ule tulimwacha dr slaa alikesha mpaka saa tisa usiku hakuna aliyepokea simu yake tena na hata anaposoma makala hii atakumbuka vizuri sana usiku ule!
Siku iliyofuata kila mmoja alikuja na sababu zake za uongo ili mradi wajumbe waliokuwa wakisubiri kikao ambao wote walikuwa watumishi wa makao makuu waamini.
Hakuna anaejua wale maghaidi feki waliishia wapi!
KWA HIYO MSIONE VYAELEA MJUE TU VIMEUNDWA









  SAKATA LA SAED KUBENEA KUMWAGIWA TINDIKALI

Ndugu Wananchi,
Baada ya mkakati wa kujiteka kukwama Mbowe hakukata tama, aliandaa timu mpya ya kazi ya kukifanya chadema kuhurumiwa na kukifanya ccm kuchukiwa,

Mbowe alimpa Mnyika jukumu mpa la kuandaa vijana wenye uwezo wa kuteka kiukweli na sio waigizaji tena, wenye uwezo wa kuteka kudhuru na hata kuua,
Mnyika kama alivyotajwa na gazeti Fulani kuwa ni mwanachama mtiifu wa Mbowe alitimiza agizo hilo haraka na kukabidhi hadidu za rejea kwa Mbowe,

Timu yake ya utekaji iliundwa na watu wafutao:-
1.     Sabra  aliyepewa jina la kazi kama VX (i) (mlinzi wa makao makuu chadema) badae akapewa kuwa mkurugenzi wa ulinzi, huyu bwana aliwahi kutumikia jeshi la magereza na sasa ni msaidizi wa bwana Rwakatare,
2.     Deus mallya au Deus Aman VX(ii) huyu atakumbukwa kwa tukio la Chacha Wangwe na inaweza kuwa ushahidi wa kifo cha utata cha marehemu Wangwe.
3.     Henry Kilewo VX (iii) huyu atakumbukwa kwa tukio la kutekwa kwa kijana wa Igunga na kumwagiwa tindikali
4.     Kasha walikuwepo wasaidizi wao walioitwa ‘WATINDI’ ikimaanisha wabeba tindikali
Kikosi kazi hiki kilofanya organization kwa umakini sana na kilifanikiwa vyema kabla ya mmoja wao kutoboa siri kwa wahusika waliodhurika.

Siku ya tukio kulizuka mabishano kati ya Mnyika na Deus Mallya kuhusu malipo yaliyokuwa yamebaki.
Mnyika alipewa majina ya vijana wao ‘watindi’ ili awalipe pesa ya awali yaani advance,
Aliwalipa kila mmoja Tsh 300,000/= na baki yao iliwa Tsh 200,000/= kila mmoja,
Wakubwa wao yaani akina sabra na deus walilipwa Tsh 700,000/= kama advance na baki lao likiwa 300,000/= kila mmoja.

Wakati huo mbowe na mkurugenzi wa pesa makao makuu ya chama bwana Antony Komu (mmiliki wa gazeti la MwanaHalisi) walikuwa katika mahusiano mazuri kabisa yasiyo na migogoro,
Mbowe alikuwa tayari kashawapa target ya kupiga ili wananchi wapate hasira na kuichukia serikali ya chama cha mapinduzi ili pia iwe namna ya wao kutafuta njia mbadala ya kisiasa ambayo aliamini ni chadema,

Vijana walipanga mipango na kufanikiwa kumwagia saed kubenea tindikali waliyoipata toka kwa mbowe mwenyewe na akijua alipoipata mwenyewe.
Baada ya mpango ule kufanikiwa na Saed Kubenea kupata nafuu, chama hakikupata mrejesho ambao mbowe aliutarajia, badala yake waandishi wa habari waliiteka ile issue na kuwa ajenda ya jukwaa la wanahabari na sio la chadema kama ilivokuwa imetegemewa.

GHAIDI MMOJA AJILIPUA KWA ANTONY KOMU
Wakati issue ikishika kasi mmoja wa wale maghaidi aliyekuwa amepunjwa pesa zake na kiongozi wao aliamua kumatafuta Sabra mguu kwa mguu,
Sabra hakuwa na majibu yenye adabu badala yake alikuwa akimtolea vitisho vingi vya kutishia maisha yake,
Bila hiyana kijana aliamua kujilipua akamfuata Kubenea na kumpa mkanda wote ulivyokuwa na akampa ushahidi wa sms na hata akajaribu kumtumia sms Sabra ili kubenea aone itajibiwaje,
Kubenea alipigwa na butwaa baada ya sabra kujibu kuwa ‘hata ukienda polisi wewe ndiye utashughulikiwa kwa kushiriki njama za kumwagia mtu sumu sisi tutakanusha na tena hujui mbowe ni nani wewe cheza utapotea’
Kubenea aliamua kumshirikisha boss wake yaani Komu,
Komu alimtafuta Mbowe kwa jazba sana na kumuomba wakutane kuna jambo la hatari kamfanyia,
Mbowe alikubali wito wa Komu kwa hofu kubwa kwani alijua deal limesanuka,
Alimfuata nyumbani kwake Tegeta alipowakuta wapo wote kubenea na komu pamoja na kijana Yule,
Baada ya kupewa mkanda mzima mbowe aliinuka na kutoa Tsh 300,000/= na kumpa Yule kijana na kumuomba wawasiliane ili ampe kazi ya kufanya na sasa kijana huyu ni baunsa wa billcanas club pale anaitwa SWAI.
Mbowe aliamua kumuomba radhi Komu na kujieleza ajuavyo mwenyewe lakini wakawekeana yamini ya kwamba Mbowe atachangia uchapishaji wa MwanaHalisi matoleo 10 na kumpangishia kubenea Nyumba nzima yenye mkataba wa miaka miwili.

Wengi huwa wanajiuliza kwanini kubenea anashindwa kuwabaini waliomteka na kummwagia tindikali mpaka leo?
Majibu ni hayo.
MBOWE SIO BINADAMU WA KAWAIDA KABISA,
HATA MIE NAOGOPA KUWEKA HADHARANI JINA LANGU KWA SABABU NAJUA NAWEZA KUFA WAKATI WOWOTE KWA MANUFAA YAKE

3 comments :

  1. Duh leo ndio kwanza nimeufungua mtandao huu na nilichokiona ni kuwa ni moja ya mitandao inayoendekeza ujinga,uongo na propaganda zilizopitwa na wakati.
    Kwaherini

    ReplyDelete
  2. Taarifa kama hii ni furaha kwa wapumbavu.

    ReplyDelete

 
Copyright © 2013. BongoAfrica - All Rights Reserved.