Thursday, November 21, 2013

PROFESA LIPUMBA : NIKO TAYARI KUACHIA UWENYEKITI WA CHAMA CHA CUF



 

 
WANA - BONGOAFRIKA HII NI NUKUU YA GAZETI LA RAI KUTOKA KWA LIPUMBA ILIYOWEKWA KWENYE MTANDAO WA JF NA MWANACHAMA WA JF KAMA AMBAVYO BONGOAFRIKA IMEZIANSA


Kama ilivyo kawaida yangu, nilipokuwa napitia gazeti moja la kila siku la Rai, nilikutana na habari iliyokuwa na anuani Prof. Lipumba: Niko tayari kuachia Uenyekiti CUF,katika habari hiyo kuna nukuu ya maneno ya Prof Lipumba ambayo anasema "watu wenye sifa ya kukiongoza Chama wajitokeze kuwania nafasi mbalimbali hata hii ya uenyekiti, mimi bado sijachukua maamuzi yoyote ya kutaka kugombea uenyekiti"

Nikiwa kama mwanasiasa kijana tena kiongozi ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) niliipitia habari hiyo kwa umakini mkubwa. Nilikuwa na sababu ya kufanya hivyo; kama ifuatavyo.

i) Nikiwa ni mtumishi na kiongozi wa taasisi ya kisiasa ni wajibu wangu kuelewa na kufuatilia habari za kisiasa ili niwe na ufahamu wa kutosha na weledi katika field husika.

ii) Kulingana na hali ya kisiasa nchini, hasa siasa za mivutano, mitafaruku, unyanyapaa na vita inayoendeshwa na wapinzani wa Chama Cha Mapinduzi hapa nchini, siasa zinazotokana na uroho wa madaraka, upangaji safu, ukanda, udini na Ubinafsi.

Taarifa hiyo ikanipa mwangaza mpya juu ya mwenendo na hatima ya Chama Cha Wananchi (CUF) kama chama cha siasa, ambapo uamuzi wa Mwenyekiti wake wa sasa unatoa fursa na kukaribisha ushindani kwa wanachama wa chama hicho kuwania nafasi yake na kwamba hatua hiyo inaimarisha DEMOKRASIA YA KWELI sio tu kwa Chama husika bali hata kuwa mfano kwa Vyama vingine vya Upinzani ambavyo demokrasia yake ni tete na haijastawi ipasavyo.

Natumia fursa hii kupongeza hatua hiyo, ni pongezi binafsi si za jumuiya yangu na kwamba pongezi zangu nimezieleza znatokana na msingi wa hayo niliyoyaeleza hapo juu kwa ufupi.

Umefika wakati vijana kuamka na kujitambua, ni wakati wa vijana kuzitafuta, kuzipata na kuzitumia fursa kila zilipo ili tuweze kupata mafanikio binafsi na kuleta maendeleo kwa jamii yetu. Hivyo fursa popote ilipo, iwe kwenye siasa, uongozi, biashara, michezo na kadhalika ni wakati wa Vijana kuzitafuta na kuzitumia, mimi nikiwa kama mwanasiasa na kiongozi wa taasisi ya kisiasa naziona fursa za kisiasa zaidi na ndio maana natoa pongezi kwa Prof Lipumba kwa uamuzi wake na kutoa wito kwa Vijana wenzangu kujipima na kujitathmini kisha kujitokeza kugombea nafasi hiyo.

Nafasi hiyo ama mfano wa hiyo ambazo sehemu nyingi katika mashirika na taasisi zimekamatwa na wazee, lakini hii haina maana kuwa hakuna vijana wenye uwezo na weledi wa kushika nafasi hizo, natoa wito kwa vijana kujiamini na kuonyesha ufanisi na Uzalendo katika utendaji wao ili waweze kuaminika na kutosha kukamata nafasi hizo, ili halitatokea kwa urahisi ni lazima kutakuwa na Class struggle na kwa sababu kulingana na population yetu kama nchi mtaji wa maendeleo ya nchi hii na kundi lenye nguvu ni vijana, na kwa kutojitambua vijana wanapambanishwa wao kwa wao na kutumika na wazee ili kumkandamiza kijana mwenzao ambao anaonekana kutishia maslahi na nafasi za wazee kwenye taasisi fulani ya siasa. Nikiwa muwazi zaidi nadhani inawezekana nikaonekana biased kwa kuwa sitokani na chama hicho lakini nataka nieleweke kuwa VIJANA WANASHIKISHWA SIME ZA KUANGAMIZA VIJANA WENZAO BILA KUFAHAMU KUWA HAO NDIO ICON NA WAWAKILISHI WAO.

Kama tunaamini katika Demokrasia ni lazima tuache demokrasia hiyo itawaliwe na haki na Uwazi. Ni lazima tukubaliane hata kutokukubaliana ili demokrasia yetu ikue na itutoe hapa tulipo kwa usalama na amani. Malumbano, vitisho, kejeli, kuchafuana na hata kutishiana uhai hakutatufanya kuwa Taifa la watu wenye hekima na busara. Hatubaki Salama na kuendelea kuwa kisiwa Cha AMANI.

Vijana lazima tujitambue, na tutambue kuwa future ya Nchi hii ipo mikononi mwetu na sisi ndio tutakaoamua TANZANIA yenye NEEMA ama yenye LAANA.

Vivaa Vijana Vivaaa....!

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2013. BongoAfrica - All Rights Reserved.