Monday, November 25, 2013

MAKALA YANGU KWA GAZETI LA MWANAHABARI LA LEO...!!



Wapo wanaodhani kuibadili nchi kimfumo wa utawala ni kuondoa chama tawala na kuweka kingine bila transformation ya fikra na mfumo wa utawala ndani ya jamii na ndani ya vichwa vya watu wanaojiita/wanaojidhania ni viongozi, (hapa shule kubwa sana inahitajika), lakini tukienda kwa lengo la kuitoa ccm tu madarakani kwa aproach ya now and then, tukidhania kuwa lengo letu namba moja ni kuitoa ccm madarakani bila kujali jamii haina wala haijajua tofauti ya taifa na vyama vya siasa, bila jamii kubadilishwa kimtazamo na kiwajibu, bila mifumo ya kiuongozi kubadilishwa, kesho ataibuka mwingine na kuwahadaa kwa style hiyo hiyo na tutajikuta tunajipeleka shimoni.
Haitakuwa tofauti na wasanii waliopata hasira kwa kuona unyonyaji umezidi katika sanaa na kuwahamasisha wasanii wenzao kuanzisha movement kubwa ya kupigana na wanyonyaji, lakini katikati ya vita vyao wakatokea wajanja zaidi yao waliotumia njia kama yao na kuwahamisha wasanii wenye ushawishi kasha movement yao ikafia mbali.
Mwisho wa yote tunajikuta tumekusanya watazama show na wacheza show kwenye makundi ya siasa.
Watazama show  ni watu wenye ufahamu kuhusu sanaa au muziki, ao hukaa au husimama kando bila kucheza wala kelele zozote, hutamani kumwona msanii akiimba na kucheza kwa kiwango halisi, asiende nje ya ufunguo wa kuimbia, sauti isikwame wala asianze kukohoa hovyohovy jukwaani.
Hutamani kumwona msanii akianza kutumbuiza mwanzo mpaka mwisho bila kuonesha dalili ya kuchoka ili mradi tu atimizia hitaji la kuimba kwa kiwango kinachostahili, ndiyo raha ya watazama show nikiwemo mimi.
Endapo msanii akikosauwezo huo niliouleza hapo juu, pengine kwa kukohoa, watzama show hudhani amepaliwa tu na anaweza kukaa sawa na kuimba vyema, au akienda nje ya mstari wa ufunguo huwa wavuimilivu na hujitengenezea sababu zao za kujifariji na kutegemea atarudi kwenye ufunguo na ataimba vyema.
Lakini akidumu katika uhafifu huo wa kimuziki, watazama show huanza kuguna na pengine hujiuliza kama msanii anafanya makusudi au hayuko serious na kazi yake.
Mara wanashangaa msanii anaishiwa pumzi na kuanza kulazimisha wanyanyue mikono hewani akiwaambia…mikono… mikono…mikono… hali hii huwakera watazama show na huamua kuondoka bila kujali muda wao na gharama walizotumia kufika hapo, wanaamua bora wakalale kuliko kukwazika.
Watazama show wakikosa ladha ya burudani waliyotarajia huondoka bila kujali wamelipia kiingilio getini, huamua kurudi kulala wakitarajia kuota ndoto zenye kuwatia moyo, kuliko faraja waliyoitegemea na kuikosa kwenye show,
Kadhalika kwenye makundi ya wanasiasa wapo wasanii hodari wa kuyamudu majukwaa kuanzia kwenye hoja mpka kwenye propaganda, kwa kundi la watazama show kwenye muziki kwenye siasa tunawaita wachambuzi wa hoja za kisiasa, hawa hujali sana kuona mtu anaeongelea issues na sio propaganda pekee na kusahau kutoa suluhu ya matatizo hata kama yeye sio serikali lakini jukwaa ni sehemu ya yeye kutolea ushauri kwa serikali akichanganya na propanda ili angalau wananchi wamwone anafaa.
Huyu mwanasiasa akienda nje ya ufunguo huu huwapoteza watazama show wa kisiasa na hubaki na wacheza show kama nitakavyoelezea hapa chini.
Wacheza show wao ni wabaya sana, maana wao hucheza sambamba na msanii anapoimba jukwaani, msanii hujikuta akiendeshwa na wacheza show  walio kwenye dancing flow ambao hata hakufanya mazoezi ya show pamoja nao.
 Wacheza show huamua hata kumlazimisha msanii aimbe wimbo fulani ambao hata hakujiandaa nao, (Mtakumbuka 2006 Shaggy alipokuja diamond jubilee kilichotokea)
Hawa maDisco Bugerz wakikosa kuheshimiwa na msanii kwa kile wakitakacho huamua kupiga fujo na hata kumrushia chupa au matusi.
Kadhalika kwenye siasa kuna kundi hili la wacheza show wanaopenda kusikia mwanasiasa akiwananga wanasiasa wenzake kwa zaidi ya dakika sitini (60) au zaidi akitembelea nyota au maneno ya wenzake au makosa ya wenzake kila jukwaa haongelei issue zaidi ya Fulani alisemakitu hiki au kile, au mimi nitapambana na Fulani mpaka ang’oke au Fulani ni mwizi au fisadi au serikali imekosea hiki bila yeye kusema nini kifanyike.
Wacheza show wa siasa hufurahi sana kila anapoongea kwa namna hii, lakini ipo siku wanakutana nae huyu mwanasiasa aliyezoea kutembelea nyota ya wenzake akakosa kuwanga hapo wacheza show ya siasa huanza kusema siku hizi huyu jamaa akachuja hana kasi kama zamani, kumbe kilichobadilika ni kwamba leo ameongelea issues na sio watu hapo ladha yao waliyoizoea hupotea kabisa.
Hali hii imesababisha wacheza show  wengi kuwa wafuasi wa wanasiasa wa aina ya kizazi cha akina feruz wasiowaza kuhusu mabadiliko ya mifumo, ni wanasiasa wanaowaza katika kubandua mwanasiasa Y na kuweka mwasiasa X bila kuchora upya msitari wa utawala na mfumo wake.
Inatokea wakati wansiasa wa aina hii wanapata wakati mgumu majukwaani au kwenye mijadala wanapokutana na wenye hoja kinzani zinazojadili issues badala ya wao kujaribi kujibu hoja kwa hoja hubadilika na kufanana na wasanii wa kizazi cha akina Diamond wanapoishiwa pumzi utawasikia wakisema ..weka mikono juu…oyoooo… mikon mikono mikonooo…
Na kwa sababu wacheza show wanapenda aina ya hamasa aliyonayo msanii huinua mikono juu na kumpigia makofi kwa shangwe kubwa.
Lakini hufikia wakati mashabiki hawa kwa kuwa hawajajengwa kimfumo huhama na kumfuata msanii mwingine atakaekuwa na hamasa kubwa zaidi ya huyu kwani wao wanachokifuata ni hamasa na sio msingi wala mfumo.
Kwa tafasiri rahisi wanasiasa hawa huhama kwenye mada na kuanza kwenda na aina ya usemaji waliozoea majukwaani kwa kuwataja watu na kuanza kutafuta kupigiwa makofi na wananchi ya kishabiki.
Hata kwenye siasa pia hufikia mahala wacheza show wa siasa wakamwona mwanasiasa mwingine mwenye domokaya kali zaidi na mwenye Kiswahili cha pwani namisemo ya umakuini na bi kilembwe na kumfuata wakimwacha wa awali kwa sababu wanataka nahau na vijembe vipya sio mfumo wala misingi.
Mifumo ya kiutawala ni lengo namba moja, kubadilisha mifumo inayosababisha wizi wa mali za umma, mianya inayosababisha rushwa, mianya inayosababisha uonevu n.k
Sio kuahidi kuwafunga watu au kuwachukulia hatua wenye tuhuma za wizi huku mifumo ikibaki vilevile, je uhakika wa kupata watu waaminifu kwenye mifumo iliyowapa watangulizi wako mianya ya wizi uko wapi?
Huwezi kuamini katika mabadiliko ya mtu pasipo mfumo kubadilika kwanza, tunatamani kuona viongozi wanaodhani wanaweza kuwa mbadala wa hawa waiopo wakijipambanua kwa mifano halisi ya nafasi zao walizo nazo katika taasisi zao kwanza.
Mjue kwa sasa watazama show ni wengi kuliko wacheza show, hawa watzama show huwa makini sana na endapo utaenda nje ya key watajua na hawatapiga kelele, ukirudia tena watajiuliza..je ni makusudi au kajisahau, au katuona tumekuja humu kumshangaa yeye na sio show?
Wakianza kujiuliza maswali hayo uwezekano wa kuondoka bila kujali muda wao waliopoteza kwako ni mkubwa mno.
Wacheza show wao watakuzomea na pengine usipojirekebisha watakupiga na kukuabisha.
Siasa haiko hivyo bali tunasimama leo kwa ajili ya kesho, na sio kusimama mchana wa leo kwa ajili ya jioni ya leo, Mobb politics huvuma kwa wakati wa rika na huisha rika linapokwisha.....!!
NATAMANI RIKA LA UHITAJI HILI LITAKAPOPITA TUBAKI KWA LENGO MOJA KUU NALO NI KUJADILI NA KUPANGA KWA AJILI TAIFA LETU

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2013. BongoAfrica - All Rights Reserved.