Sunday, November 24, 2013

KUKIRI KWA DR MKUMBO NA YALIYO NYUMA YA PAZIA


 

Jana muda na wakati kama huu ndio nilisema itakuwa mwisho kuandika kuhusu mambo ya kipuuzi yahusuyo chadema...nimesema mambo ya kipuuzi tu na sio hata ya maana, mambo ya maana kuhusu chadema nitaandika lakini ya kipuuuzi yatokanayo na chadema sitaandika,
Sasa kabla ya kutimia saa 24 kukamilika kwa muda wa siku nzima niliyoisema yaani tokea jana mapka leo muda huu, naomba kuhitimisha kama ifuatavyo.

Kwanza kabisa katika hili sakata tumekwazana sana, tumefikia hatua tumedhaniana kuwa ni maadui wakubwa, lakini hii yote ilikuja baada ya kuona chama kinaka kimya kwa tuhuma zinazosambazwa kwa makusudi ili kuuchafua upande fulani wa watu wahisio ni tishio kwao kwenye hoja za chama,

Uongozi ulikaa kimya lakini ilipofikia hatua uzushi ule ukawarejea wao wenyewe na kuanza kuwachafua wao walijitokeza haraka sana kuukana,

Hii inaonyesha walifurahia na kuvizia pengine hila na mpango wa kudhoofisha upande walioulenga ungefanikiwa kitu ambacho kilifeli,

Jana Dr Mkumbo alikiri na alieleza kiundani maana halisi ya kushiriki kuandika waraka ule wa ushindi unaoitwa waraka wa uhaini,

Wapo watu wanaolaumu na kuhukumu kwamba mikakati ile ya siri haitakiwi kwa sababu uchaguzi haujatangazwa na katiba hairuhusu,.. naomba nieleze hili kwa mifano halisi...

Chadema na vyama vyote vya siasa tanzania hasa vya upinzani, tangu mwaka 2010 vimekuwa na mikakati ya ndani na ya siri na mingine ya wazi ya kupanga namna ya kujipanga kuikabili ccm 2015,

Kila chama kina namna yake hasa chadema kinayo mikakati mingi na ya siri ambayo hata sio wanachama wote hata wale wa makao makuu wanaitambua,

Lakini wakati hayo yakiendelea tume ya uchaguzi haijatangaza uchaguzi, wala hakuna sehemu inaruhusu kuwepo kwa mikakati hiyo ya siri ya ndani ya chama mradi tu haivunji sheria za nchi wala katiba ya nchi,

Kadhalika ndani ya chama ikiwepo watu wanaoamini kuwa mabadiliko ya uongozi yanhitajika lazima wawe na mikakati maalum yenye umakini mkubwa na usiri bila kukigawa chama maana mikakati yao ni ya siri yao ya kupanga mikakati yao ya ushindi tu, na ndio sababu hawakuifanya public lakini watawala wa chama ndio waliousambaza waraka huo kuharibu chama kwenye public wakidhani wanamharibu mtu mmoja au kikundi fulani,

Ikiwa chadema inaamini kuwa ccm imechoka na kunahitajika mabadiliko ya uongozi kuanzia mfumo mpaka figures na wanapanga mikakati ya wazi na ya siri bila kuharibu wala kuwagawa watanzania, basi wawe tayri kukubali kuwa hata kwenye taasisi hili kufanyika ni halali kabisa,

Chadema imefanya makosa makubwa sana kuanza kusambaza habari kwenye public kuanzia ule waraka wa ''HEKAYA YA DOMOKAYA FEKI'' uliosambazwa na Kiongozi kwenye blog zake na kiongozi mwingine kugonga like,
Vyote hivi vinadhihirisha kuwepo kwa miakakti ya upande wa pili bila kuzingatia wataharibu sura ya chama wakidhani wanamharibu mtu mmoja au kundi moja,

Hapa napata tofauti ya siasa za mikakati ya mihemko/matukio na siasa za mikakati za misingi na za kisayansi,

Zitto na Mkumbo jana walimaliza utata mkubwa wa kukomesha tamanio la wahafidhina waliotaka ahame au asuse kama waraka fulani uliowekwa humu mitandanoni ukionyesha team moja iliyojumuisha wabunge wanne iliketi na kiongozi mmoja wakipanga namna ya kumfanya Zitto asuse ajisababishie kufukuzwa au kusimamishwa uongozi ili akose sifa ya kugombea wenyekti.

Napenda kuwaomba watu wote wanaojihusisha na siasa kuwa usijidanganye kutopanga safu ya mikakati mapema ikiwa una nia ya kugombea ukisubiri uruhusiwe...

Binafsi nampongeza sana KAKA YANGU DR MKUMBO NA KAKA YANGU ZITTO kwa kuonyesha tofauti kati ya mikakati ya wasomi na mikakati ya kihafidhina isiyojali misingi na dira ya taasisi!!

Ombi kwa upande wapili unajiandaa kutoa majibu, leo nimemuona Msigwa na Sugu wakiandika kwenye fb kwa mihemko mikubwa wakirudia kosa lilelie walilolifanya awali la kushambulia taasisi wakidhani wanamshambulia mtu mmoja, mfano jana zitto na kitila walionyesha tofauti yao na wale walioanza kuwashambulia na kuwagwa wanachadema, lakini akina zitto walirudisha watu kuwa calm, leo Msigwa ameamka saa 11 alfajiri na kukimbilia facebook na jf na kuanza kufanya ujinga wa aina ile ile ya kutaka mpasuko,

Najua uwezo wake msigwa na sugu, najua vikao vinapokaa ndipo wanapopata cha kuja kusema public lakini kwa hili la leo wameharibu kabisa hawajatumia uwezo wa uono wala busara,

Viongozi wakuu mtakapokuja kujibu hoja za akina zitto msifanye kosa kama la awali la team iliyokutana gizani na kupanga hekaya feki, bali mpigilie msumari wa umoja na mshikamano,

Kinyume cha hapo wengi wataanza kuamini maneno yasemwayo kwnye mitandao na mitaani kuwa Mzee meti ameamua bora CHAMA KIFE KIBAKI NA WABUNGE 3 KULIKO KURUHUSU MTU ASIYEMFAHAMU KUWA KIONGOZI,

Ikifikia hapo je tuamini kuwa lengo la kutwaa dola 2015 limekufa kwa sababu sio sahihi kuipata dola mkiwa nje ya mirija ya kunyonyea pesa ? au lengo la kuwafanya watu walie na wabaki yatima na vilema wakipambana ili cdm ipate hatamu ni nini?


KWA HAYO NIMEMALIZA.....NYAKARUNGU GRAYSON MANYORI

SERENGETI NAGHUSI NATTA
0755 023 503,
diplomatictable@gmail.com

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2013. BongoAfrica - All Rights Reserved.