Saturday, November 16, 2013
HUYU KIJANA, AU HUYU MZEE NANI ANAFAA KUWA KIONGOZI?
UJANA, UZEE NA UONGOZI!!
Kijana yeyote mwenye maono, mwenye hekima ya kusikiliza, mwenye upeo wa kutafakari jambo, mwenye kujali, asiyeweza kulewa sifa, asiye na ushamba wa mafanikio.
Anaweza kuwa kiongozi wa taifa lolote Duniani na likafanikiwa kwa maelekezo yake yeye akiwa mkuu wa nchi.
Umri na uongozi vina mahusiano lakini sio kila kijana anasiafa ya kuwa kiongozi.
Uzee ni sifa ya sio sifa ya uongozi, bali tunakuwa na nafasi ya kupima mzee kwa historia yake ya uongozi huko nyuma, hata wazee na vijana wanaweza kuwa na sifa ya kuwa viongozi wazuri na wote pia wanaweza kukosa sifa ya kuitwa viongozi wazuri.
Umri una nafasi katika kupima matukio ya mtu ya nyuma kwa sababu alishapata kutumikia siku nyingi tofauti na kijana kwani hana historia ndefu ya kupimwa.
Wapo vijana wenye historia ndefu ukilinganisha na umri wao, historia hizo znawapa sifa kubwa ya kuwa viongozi ukilinganisha na wazee watakaosimama nao.
Wapo wazee wenye umri mkubwa sana wasio na historia ya kulidhisha ya uongozi bora ukilinganisha na umri wa uzoefu wao.
*ANGALIZO* Hii mada iko kama ilivyo, kwa ajili ya watu kuelewa mantiki ya umri kwenye uongozi sijamlenga mtu, na ikiwa hujaelewa bora usikoment kabisa*
Wenu Nyakarungu, G. 'UTASHI NI MTU'.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment