Wednesday, November 20, 2013

DAVID KAFULILA : NAJUA SIRI YA MASHINE ZA TRA...Soama Zaidi hapa chini

UCHUNGUZI WA KINA UNAHITAJIKA MASHINE ZA EFDs. 
 
 Leo kamati ya uchumi, viwanda na biashara tumekutana na TRA Kuhojimmgogoro baina yao na wafanyabiashara. Maoni yangu ni yafuatayo;
1. Kati ya wafanya biashara wenye kulipa kodi Tanzania ambao wanafikia 1.5millions, wafanya biashara wanaostahili kutumia mashine ni laki mbili tu. kwa maoni yangu kwanza kwa ujumla hiki ni kiasi kidogo sana, kwani kwa mujibu wa ripoti ya IMF ya mwaka 2011 kuhusu sekta isiyo rasmi na kodi, Tanzania wanaostahili kulipa kodi ni milioni15 huku wanaolipa ni milioni1.5..na zaidi kwa ku target watu200000 kwa kuanzia kuingizwa kwenye mfumo wa mashine bado tupo nyuma sana.sehemu kubwa ya biashara ipo nje ya mfumo na hivyo hailipi kodi.

2, nikweli mashine hizi kwa namna ya utaratibu ulivyo bado ni TRAmwanaozinunua kwani wanamrudishia mfanyabiashara kwa kuhesabu manunuzi ya mashine Kama sehemu ya kodi. Kama mtu alipaswa kulipa kodi milioni 1 kwa mwaka lakn alinunua mashine ya laki Sita basi atalipa kodi ya laki nne tu badala yanmilioni1, kasoro ya utaratibu huu unafanya mfanyabiashara atumie pesa alokuwa anazungusha kununua mashine. Mimi nilipendekeza kuwa TRA wangenunua mashine na kugawa au wangeipa kampuni inunue mashine na kuzigawa kwa utaratibu kwamba kampuni husika italipwa na TRA, Ile pesa ambayo TRA wanamsamehe mfanyabiashara kwa kununua mashine basi wasimsamehe na badala yake waielekeze kwa alogawa mashine na kodi ibaki Kama kawaida. Hii ingeondoa malalamiko ya wafanyabiashara kutumia mitaji Yao kununua mashine.

3. Hizi mashine kwa namna yeyote bei yake ni kubwa na ni mzigo kwa serikali. Bei ya mashine hizi nchini china ni Kati ya dola 80 mpaka dola 140, TRA wanasema mashine hizi zinatengenezwa kwa namna ambayo inazifanya ziweze kuwasiliana na TRA lakn wameshindwa kuonesha programme hizo zinaongeza gharama kiasi gani ili mtu anunue mashine kokote lakn awekewe programme hizo kwenye mashine na TRA ili mashine yake iweze kuwasiliana na TRA. Hii ingesaidia UWAZI kujua kiasi gani kinatumika kununua mashine na kiasi gani kinatumika kuingiza programme pamoja na matengenezo ili tujue msingi wa tofauti ya bei.

4.Sababu nyingine ya bei kuwa kubwa ni kodi ambazo mashine hizi hutozwa zinapoingizwa nchini, kwakua mashine hizi ni kwajili ya TRA kuongeza ufanisi wa ukusanyaji kodi mashine hizi zilipaswa kufutiwa kodi kwani ni aibu tunasamehe kodi zisizo na msingi lakn vifaa Kama Hivi vinatozwa kodi na kuongeza gharama.

Sababu nyingine ya gharama ni sheria ya manunuzi ambayo siku zote inafanya serikali kununua vitu kwa bei Mara tatu ya bei halisi na bado serikali haitaki sheria hii ifanyiwe marekebisho na hivyo imebaki kwa faida ya wanaofanya biashara na serikali. Hivyo kwakua mashine hizi zimenunuliwa kwa kufuata sheria hiyo ni wazi bei itakuwa sio chini ya Mara mbili ya bei halisi. Mchanganyiko wote huu ukiambatana ukosefu wa UWAZI unahitaji uchunguzi kwani biashara ya mashine laki mbili ni zaidi ya billioni 100,usiri mwingi kwa biashara kubwa Kama hii unacha mashaka matupu kuhusu bei.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2013. BongoAfrica - All Rights Reserved.